Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imewataka wakulima na jamii kwa ujumla watumie Mbegu zilizothibitishwa ili kuongeza mavuno tija na kipato.
Hayo amesemwa Mkurugezi mkuu wa Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania Patrick Ngwediagi Wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini dodoma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mwaka wa fedha 2022/2023 na mwelekeo wa utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/2024 ya taasisi hiyo.
Amesema kuwa zaidi ya shilingi bilioni 12 zimetengwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya kuendelea na uboreshaji wa shughuli za uthibiti na usimamizi wa ubora wa mbegu pamoja na utekelezaji mradi wa kuendeleza sekta ya kilimo na uvuvi ( AFDP) kwa kujenga Maabara ya Mbegu.
Aidha amesema kuwa jukumu kubwa la Taasisi hiyo ni kusimamia shughuli za uzalishaji wa Mbegu na biashara ya Mbegu Ili kuhakikisha wakulima na Wadau wengine kuwa Mbegu wanazouziwa zenye Lebo ya TOSCI ni sahihi kwa matumizi.
Pia amesema kuwa matumizi ya Lebo za ubora za TOSCI kumesababisha kupungua kwa tatizo la uwepo wa Mbegu feki na zilizo na ubora hafifu hapa nchini.
No comments:
Post a Comment