Tuesday, October 13, 2026

*MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA SAID YUSUF GOHA*

Na Dkt. David Mramba

Malinyi - Morogoro. 

Leo *Tarehe 13/10/2026* Mamia ya Watanzania kutoka katika baadhi ya Mikoa wakiwemo Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali wamejitokeza kwa wingi kushiriki mazishi ya *ndugu Said Yusuf Goha* aliyewahi kuwa 
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa.

MADEREVA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI WAKATI WOTE.


Madereva wametakiwa kuzingatia sheria na taratibu za usalama barabarani wakati wote wanapotumia barabara, badala ya kuzifuata pale wanapomuona askari wa usalama barabarani.

Wito huo umetolewa Oktoba 13, 2026, na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Edson Mwakihaba, wakati akizungumza katika kipindi maalumu cha elimu ya usalama barabarani kilichorushwa na kituo kimoja cha redio wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

Mwakihaba ameeleza kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani litaendelea kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa wananchi wanatumia barabara kwa usalama na kufika salama katika safari zao.

Aidha, amewataka madereva wote wa vyombo vya moto kuhakikisha wanamiliki leseni halali za udereva na kupata mafunzo katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, badala ya kujiunga na vyuo ambavyo vimefungiwa au havitambuliki kisheria.

Amesisitiza kuwa uzingatiaji wa sheria za usalama barabarani ni wajibu wa kila mtumiaji wa barabara na unapaswa kuzingatiwa wakati wote ili kupunguza ajali na kulinda maisha ya wananchi.

Monday, October 12, 2026

ATAFUTWA KWA TUHUMA ZA KUMUUA MTOTO WA KAMBO BAADA YA KUKATALIWA NA MAMA WA MAREHEMU

JESHI la Polisi Mkoani Pwani linamsaka Mkazi wa Kimara Dar es Salaam Seif Ally kwa tuhuma za kumuua mtoto wa kambo (10) kwa madai ya mama wa marehemu kumkataa.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Mkoani humo Salim Morcase amesema kuwa mtuhumiwa alitekeleza mauaji hayo baada ya kukataliwa na kuhusisha tukio hilo na wivu wa kimapenzi.

Mtoto huyo alikuwa mwanafunzi wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Lugoba Halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo alikuwa akiishi na bibi yake.

Morcase amesema kuwa taarifa zinaeleza kuwa usiku wa Oktoba 9 2026 mtuhumiwa alifika katika Kijiji cha Mboga alipokuwa akiishi mtoto na bibi yake na kumchukua mtoto huyo na kwenda naye kusikofahamika.

"lipofika tarehe 10 Oktoba 2026 mtuhumiwa huyo alimtumia bibi wa mtoto huyo ujumbe wa maneno kwenye simu yake ya mkononi akimuelekeza mahali ulipo mwili wa mjukuu wake na kumtaka kama akimtaka mjukuu wake kwenda kuchukua mwili wake katika Kijiji cha Rodi Chini Kata ya Lugoba Wilaya ya Kipolisi Chalinze,"amesema Morcase.

Amesema kuwa baada ya kupokea ujumbe huo bibi wa mtoto huyo alitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani ambalo lilifika eneo la tukio na kukuta mwili wa mtoto huyo ukiwa umetelekezwa kichakani na kufunikwa kwa majani ukiwa unatokwa na damu mdomoni. 

"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi baada ya mtuhumiwa kukataliwa na mama wa mtoto huyo ambaye waliachana miezi miwili iliyopita na mama huyo kukataa kurudiana naye baada ya kuachana kwao,"amesema Morcase.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo ili taratibu za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake kuhusiana na tukio hilo. 

mwisho.

KIMARA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KIBITI, ASISITIZA UKAMILISHAJI KWA WAKATI


MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Ndg. Ramadhan Kimara, amesisitiza ukamilishaji wa miradi ya maendeleo kwa wakati wakati akikagua ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Mkupuka yenye thamani ya Sh milioni 528 na Kiwanda cha Samaki cha Nyamisati. 

Ramadhan Kimara amefanya ziara hiyo leo, Oktoba 12, 2026, wilayani Kibiti, akianza na ukaguzi wa ujenzi wa shule hiyo iliyopo Kijiji cha Mkupuka. 

Akiwa eneo la ujenzi, amezungumza na fundi pamoja na msimamizi wa ghala la vifaa vya ujenzi, akiwataka kuhakikisha vifaa vinatumika kwa usahihi na kwa malengo yaliyokusudiwa na kumtaka fundi kukamilisha kazi ndani ya muda uliowekwa kwenye mkataba. 

Aidha, amemtaka Mhandisi wa mradi kufika eneo la ujenzi mara kwa mara ili kufuatilia maendeleo ya kazi na kutatua changamoto zinazoweza kujitokeza. 

“Mjulisheni Mhandisi wa mradi ahakikishe muda wote anafika katika eneo la ujenzi ili kusiwe na changamoto zozote katika ujenzi huu,” alisema Kimara. 

Katika ziara hiyo, Ramadhan Kimara pia ameshiriki na mafundi katika ujenzi wa vyoo vya wanafunzi kwa kubeba matofali na kuyasogeza eneo la ujenzi. 

Baada ya kukagua mradi huo, Kimara alielekea Kijiji cha Nyamisati, Kata ya Salale, kutembelea Kiwanda cha Samaki na kukagua miundombinu iliyopo pamoja na kubaini changamoto zinazokikabili. 

Alijionea hali ya kiwanda na changamoto zinazohitaji kufanyiwa kazi ili kuwezesha uwekezaji huo kuanza au kuimarisha shughuli za uzalishaji, kwa lengo la kuongeza mapato ya Halmashauri na kuchochea shughuli za kiuchumi wilayani Kibiti.

Sunday, October 11, 2026

AZANIA BANK TAWI LA KIBAHA YAWEKA MIKAKATI KABAMBE YA KURUDISHA FADHILA KWA JAMII

Na Mwandishi wetu Kibaha

Uongozi wa Azania bank umesema kwamba utaendelea kushirikiana bega kwa bega na serikali ili kuweza  kurudisha fadhila kwa  jamii katika mambo mbali mbali ya kuleta chachu ya kimaendeleo katika sekta tofauti.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa Azania bank tawi la Kibaha Anna Monyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja kwa mwaka 2026 ambayo yamefanyikia katika  ofisi zao  zilizopo katika jengo la Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.

Katika sherehe hizo ambazo zimehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali,wateja wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka ambapo pia walipa fursa ya kufunguliwa akaunti zao na kukabidhiwa kadi za ATM.

Meneja huyo amebainisha kwamba lengo lao kubwa kama Azania bank ni kuendelea kuweka mipango madhubuti ya kuwahudumia wateja wao ikiwa pamoja na kurudisha fadhila kwa jamii na kuwapatia mikopo ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi.

"Kipekee kabisa mimi meneja wa Azania bank tawi la Kibaha napenda kuchukua  fursa hii ya kipekee kuwashukuru kwa dhati wateja wetu kwa kuweza kuendelea  kutuamini na sisi tupo tayari kuwahudumia,"amebainisha Meneja huyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Mhe.Silvestry Koka ameipongeza kwa dhati Bank ya Azania kwa kuweza kuona umuhumu wa kusogeza huduma karibu kwa wananchi wa Kibaha ambapo hapo awali walikuwa wakipata usumbufu katika kuifuata huduma hiyo Jijini Dar es Salaam.

Mhe.Koka amebainisha kwamba uongozi wa Azania bank umekuwa mstari wa mbele kushirikiana bega kwa bega na serikali pamoja na wateja wao kwa lengo la kuweza kuleta chachu ya uchumi.

Naye Afisa mfawidhi wa PSSF Mkoa wa Pwani  John Mwalisu ameupongeza uongozi wa  Azania bank kwa kuweza kuweka mikakati ya kupanua wigo wa kufungua matawi katika maeneo mbali mbali ikiwemo Tawi la Kibaha.

Nao baadhi ya wateja wa Azania bank waliopata kushiriki katika tukio hilo la maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja wameridhishwa  na huduma zinazotolewa na kufurahishwa na ujio wa ofisi za  tawi hilo kuja Kibaha.

           

Friday, October 9, 2026

MEYA DK NICAS MAWAZO AMEKIPONGEZA KIWANDA CHA U-FRESH KWA KUTOA MABATI 500 KWA SEKONDARI YA MWAMBISI

MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dk Nicas Mawazo amekipongeza kiwanda cha U-fresh Food Ltd kwa kuchangia mabati 500 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Mwambisi.

Mawazo ameyasema hayo alipotembelea kiwanda hicho kinachozalisha Juisi na kuwa serikali inaunga mkono wadau kusaidia miradi ya maendeleo kwenye maeno walipowekeza.

Amesema kuwa wawekezaji lazima warejeshe kwa wananchi kupitia miradi ya maendeleo ambayo ina faida kwa jamii na hiyo ni manufaa ya uwekezaji hapa nchini.

"Tunawapongeza kwa kujitolea kuisaidia jamii kwani imekuwa ikishirikiana na wawekezaji ambao wako jirani na hayo ndiyo manufaa ya uwekezaji katika suala la maendeleo,"amesema Mawazo.

Aidha amesema kuwa ujenzi wa bweni kwenye shule hiyo ni kilio cha wazazi kwa watoto wao hivyo wadau wanapaswa kusaidia jitihada za serikali kwa kujitolea kusaidia jitihada hizo.

Naye Ofisa Utumishi wa kiwanda hicho Dalama Mohamed amesema kuwa watatoa mabati hayo ili kuunga mkono serikali kwenye sekta hiyo ya elimu ili kufanikisha upatikanaji wa mazingira bora ya elimu

Kwa upande wake Mthibiti Ubora wa kiwanda hicho Noela Ngusa amesema kuwa kipindi cha nyuma kulikuwa na changamoto juu ya maji yanayotoka kiwandani hapo lakini kwa sasa wamedhibiti hali hiyo kwani maji wanayatibu hivyo hayana madhara tena.


MEYA WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIBAHA DK NICAS MAWAZO AMEKIPONGEZA KIWANDA CHA U-FRESH KWA KUTOA MABATI 500 KWA SEKONDARI YA MWAMBISI

MEYA wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Dk Nicas Mawazo amekipongeza kiwanda cha U-fresh Food Ltd kwa kuchangia mabati 500 kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Mwambisi.

Mawazo ameyasema hayo alipotembelea kiwanda hicho kinachozalisha Juisi na kuwa serikali inaunga mkono wadau kusaidia miradi ya maendeleo kwenye maeno walipowekeza.

Amesema kuwa wawekezaji lazima warejeshe kwa wananchi kupitia miradi ya maendeleo ambayo ina faida kwa jamii na hiyo ni manufaa ya uwekezaji hapa nchini.

"Tunawapongeza kwa kujitolea kuisaidia jamii kwani imekuwa ikishirikiana na wawekezaji ambao wako jirani na hayo ndiyo manufaa ya uwekezaji katika suala la maendeleo,"amesema Mawazo.

Aidha amesema kuwa ujenzi wa bweni kwenye shule hiyo ni kilio cha wazazi kwa watoto wao hivyo wadau wanapaswa kusaidia jitihada za serikali kwa kujitolea kusaidia jitihada hizo.

Naye Ofisa Utumishi wa kiwanda hicho Dalama Mohamed amesema kuwa watatoa mabati hayo ili kuunga mkono serikali kwenye sekta hiyo ya elimu ili kufanikisha upatikanaji wa mazingira bora ya elimu

Kwa upande wake Mthibiti Ubora wa kiwanda hicho Noela Ngusa amesema kuwa kipindi cha nyuma kulikuwa na changamoto juu ya maji yanayotoka kiwandani hapo lakini kwa sasa wamedhibiti hali hiyo kwani maji wanayatibu hivyo hayana madhara tena.