Wednesday, August 5, 2026

POLISI YAWAREJESHA SHULENI WANAFUNZI 114

JESHI la Polisi Mkoani Pwani limefanikisha kuwarejesha Shuleni wanafunzi 114 ambao walishindwa kuripoti shule kutokana na sababu mbalimbali.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Salim Morcase amesema kuwa jumla ya wanafunzi 573 walikuwa hawajaripoti shuleni.

Morcase amesema kuwa kati ya wanafunzi hao ambao hawakuripoti Shule za Msingi walikuwa 251 na wa Sekondari walikuwa ni 322 ambao walibainika katika kipindi hicho licha ya kuwa wanafunzi hao kuwa na wa miaka tofauti tofauti.

Amesema kuwa changamoto nyingine ni mimba za utotoni ukosefu wa mahitaji ya msingi kama vile sare za Shule na madaftari  na changamoto za kiafya na kiuchumi.

Amewataka wazazi na walezi kushirikina na viongozi wa dini na wa kiserikali katika kupambana na viashiria vya vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa watoto ndani ya jamii.


No comments:

Post a Comment