SAMWEL Mang'ombe (29) mkazi wa Wilaya ya Bagamoyo amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti mtoto mwenye umri wa miaka (10) ambaye alikuwa ni jirani yake.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Salim Morcase alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwezi Julai.
Kwenye tukio lingine Salim Masanja (33) Mkazi wa Wilayani Kibaha amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela na kulipa fidia ya shilingi milioni moja kwa tuhuma za kumdhalilisha mtoto wa kike (6).
Morcase amesema kuwa mshtakiwa huyo ni baba mdogo wa mhanga ambaye alikuwa akiishi naye nyumbani kwake na kesi hizo ni za ukatili wa kijinsia.
Amesema kuwa kesi zilizofikishwa mahakamani kwa kipindi hicho zilikuwa 117 huku kesi 63 zilisikilizwa na kumalizika ambapo kesi 48 zimepata mafanikio.
Amesema kuwa jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanapaswa kushirikiana ili kukabiliana na vitendo vya ukatili kwa watoto.

No comments:
Post a Comment