Monday, August 24, 2026

MJUMBE HALMASHAURI KUU CCM MKOA WA PWANI KUSAIDIA UKAMILISHAJI OFISI UVCCM KATA YA TANGINI

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCMNEC) Mkoa wa Pwani Alhaji Hussein Chuma ameahidi kufanikisha umaliziaji wa ofisi ya Umoja wa Vijana wa (UVCCM) Kata ya Tangini Wilayani Kibaha.

Akifungua Kikao cha Baraza la Umoja huo lililofanyika kwenye Kata hiyo mwakilishi wa Mjumbe huyo Nassoro Shomvi amesema mchango wake ni kwa ajili ya kuhakikisha ofisi hiyo inaanza kutumika.

 Shomvi amesema kuwa UVCCM ni tanuru la kupika vijana ambao ni viongozi wa baadaye wa chama hivyo lazima wawekewe mazingira mazuri ya kufanyia shughuli zao za kila siku.

"Vijana mnapaswa kukitumikia chama ili kiweze kuhudumia wananchi kwani nyie ndiyo nguvu ya chama na chachu ya jumuiya zote za chama hivyo lazima mpambanie chama wakati wote,"amesema Shomvi.

Kwa upande wake Katibu wa UVCCM Kata ya Tangini Lazaro Benjamin amesema kuwa ili kukamilika ofisi hiyo inahitaji baadhi ya vitu ili kukamilika.

Benjamin amesema mojawapo ni samani za ofisi pamoja na kumalizia vitu vidogo vilivyobakia ili iweze kuanza kutumika pia ukosefu wa mashine kwa ajili ya mradi wa uoshaji wa magari.

No comments:

Post a Comment