Wednesday, September 2, 2026

WAMACHINGA WAISHUKURU SERIKALI KUWATENGEA ENEO LA BIASHARA

WAFANYABIASHARA wadogo Mkoani Pwani maarufu kama Wamachinga wameishukuru serikali kwa kuwatengea eneo maalum kwa ajili ya kufanyabiashara.

Hayo yemesemwa Mjini Kibaha na Mwenyekiti wa Wamachinga Mkoani humo Filemon Maliga alipokuwa akizungumzia kuhusu zoezi la kusajili wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kwenye eneo la hifadhi ya barabara eneo la Maili Moja.

Maliga amesema kuwa wafanyabiashara hao wametengewa eneo lingine kwa ajili ya kufanya biashara mara utaratibu wa eneo jipya utakapokamilika watahamishiwa hapo ili kuendelea na biashara zao.

"Kama unavyoona zoezi linaloendelea na kuwasajili kutegemeana na biashara wanazofanya wakiwemo wauza mitumba, mama lishe, wauza matunda, chips na biashara nyingine,"amesema Maliga.

Amesema kuwa kutokana na uhaba wa ajira watu wengi wameingia kwenye mfumo wa kujiajiri kwa kufanya biashara hivyo hiyo ni ajira kwa kundi hilo kwani watu wanaendesha maisha yao kupitia biashara zao.

"Tunamshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kutaka wafanyabiashara wadogo nao watengewe mazingira mazuri kwa ajili ya kufanya biashara zao wakiwa kwenye mazingira rafiki hivyo kufanya biashara zao kwa uhuru,"amesema Maliga.

Aidha amesema kuwa kupitia biashara hizo wafanyabiashara hao wanaendesha maisha yao kw kujenga nyumba kusomesha watoto na kuongeza kipato na kujiletea maendeleo.

Naye moja ya wafanyabiashara wa eneo hilo Wilielmina Lazaro amesema kuwa mpango huo ni mzuri kwani walikuwa hawana eneo maalum na hapo walikuwa wakifanya kwenye eneo la hifadhi ya barabara ambapo maandalizi ya ujenzi yataanza wakati wowote. 

Lazaro amesema kuwa wanatunza familia zao pia baadhi wanakopa fedha kupitia biashara zao hivyo kuweza kukuza biashara na kujiletea maendeleo wao na familia zao.

RAIS DK SAMIA SULUHU HASSAN AMWAPISHA NYONGO KUWA MKUU WA MKOA WA PWANI

Dk Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimuapisha Stanslaus Haroon Nyongo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwenye hafla ya uapisho iliyofanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar leo tarehe 02 Septemba, 2026.


MPANGO WA KUJIANDAA NA KUKABILIANA NA MVUA ZA EL NINO

Nimeongoza Kikao cha Kamati ya Wataalam Wilaya ya Gairo kupokea taarifa ya Taasisi na Idara mbalimbali namna tulivyojiandaa na kukabiliana na Mvua za El Nino  Kabla ya Mvua, Wakati wa Mvua na Baada ya Mvua.

KIKAO hiki MUHIMU kimehusisha Taasisi za TARURA, RUWASA, GAUWASA, TANESCO, JESHI LA UOKOAJI ZIMAMOTO, JESHI LA POLICE, Udhibiti Ubora wa Elimu na Idara zote zilizopo chini ya Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.  

KAZI NA UTU, TUNASONGA MBELE.