CHAMA Cha Ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU) LTD kitagharamia gharama za huduma ya maji kwenye Shule ya Msingi Mwendapole ili kukabiliana na changamoto ya maji shuleni hapo.
Aidha chama hicho pia kitagharamia utengenezaji wa mashine ya kudurusu na kuchapishia na kompyuta mpakato ili kurahisisha kazi za uchapaji na kudurusu zifanyikie shuleni hapo badala ya kuzipeleka sehemu nyingine ambapo inaondoa usiri wa kazi za shule ikiwemo mitihani.
Hayo yamesemwa na Meneja wa CORECU LTD Mantawela Hamis wakati wa mahafali ya darasa la saba ya Shule ya Msingi Mwendapole yaliyofanyika leo shuleni hapo Wilayani Kibaha.
Pia amewataka wazazi kuwalea wanafunzi hao kwenye maadili mema mara wamalizapo elimu yao ya msingi ili wajiandae kuendelea na masomo ya elimu ya sekondari.
Awali mwalimu mkuu wa shule hiyo Rajabu Chalamila amesema kuwa mbali ya changamoto ya vifaa vya stationari na maji pia wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa uzio.
Chalamila amesema kutokana na shule hiyo kutokuwa na uzio wanafunzi wamekuwa wakitoroka na kufanyiwa vitendo vya kikatili.
No comments:
Post a Comment