Mamlaka ya Elimu Tanzania ( TEA ) imepanga kutumia kiasi cha shilingi Bilioni 8 kwa ajili ya kufadhili miradi ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini ambapo fedha hizo zitatumika kufadhili miradi 82 katika shule 81 zikiwemo shule 48 za msingi na 33 za sekondari Katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara.
Hayo yamesemwa na Mkurugezi Mkuu wa mamlaka ya Elimu Tanzania Bahati Geuzye wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini dodoma kuhusu utekelezaji wa majukumu na mwelekeo wa fedha ya Mwaka 2023/2024.
Geuzye amesema kuwa miradi hii itakapokamikika itanufaisha wanafunzi 39,484 na walimu 169 Katika shule za msingi na sekondari Ili kuhakikisha sekta ya Elimu inasonga mbele.
Amesema kuwa kwa mwaka 2023/2024 mfuko wa Elimu wa Taifa utatoa ufadhili kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu na kuwezesha ununuzi wa vifaa vya kujifunzia na kufundishia Katika taasisi Moja ya elimu ya juu Tanzania - Zanzibar ambao mradi huu umepanga kutumia sh Million 300 katika utekelezaji wake.
Aidha amesema katika kuunga mkono azma ya serikali ya kuhamishia makao makuu ya Nchi jijini dodom TEA kupitia mfuko wa Elimu ilifadhili Miradi ya shule mpya ya msingi inayofundisha kwa lugha ya kiingereza ya Msangalalee kwa thamani ya sh Milioni 750.
No comments:
Post a Comment