SEARIKALI imepanga kubadilisha kilimo kutoka kuwa cha kujikimu na kuwa kilimo cha biashara ambapo mabadiliko hayo yanafanyika kwa kuzingatia malengo ya kitaifa kama yalivyoainishwa kwenye dira ya taifa ya maendeleo 2025 na kuhakikisha kilimo ichangie ipasavyo Katika vita dhidi ya umasikini na kulenga kukuza sekta hiyo kufikia asilimia 10 ifikapo Mwaka 2030.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Pindi Chana katika ufunguzi wa kongamano la zao la Mtama Jijini Dodoma kwenye maonesho ya nanenane.
Chana amesema kuwa mipango hiyo yote ya kitaifa imeweka mkazo kwenye mapinduzi ya viwanda na kubainisha sekta ya Kilimo kama mhimili imara utakaowezesha upatikanaji wa maligrafi za viwanda.
Amesema kuwa Mikoa ya kanda ya kati kama iliyo kwa Nchi na Dunia nzima inakabiliwa na mabadiliko ya tabia Nchi ambapo Mkoa wa Dodoma na Singida imeamua kwa dhati kuendeleza zao la Mtama ambalo limekuwa likistawi vizuri kwa hali ya hewa ya Mikoa hiyo.
Kanda ya kati imeamua kufanya uhamasishaji kupitia kongamano Hilo kuhusu matumizi ya teknolojia Bora Katika uzalishaji wa Zao la Mtama lengo likiwa ni kuunga mkono na kutekeleza kwa vitendo jitihada za Dkt. Mhe. Samia Suluhu Hassan Katika kuongeza Kasi ya ukuaji wa sekta ya Kilimo kutokana na kuhakikisha usalama wa chakula na kipato kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment