Sunday, August 20, 2023

COREFA YAZINDUA KITUO CHA SOKA KWA VIJANA KIBAHA


CHAMA Cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA) kimezindua kituo cha michezo kwa vijana chini ya miaka 17 kikiwa na lengo la kuibua na kukuza vipaji vya vijana ndani ya mkoa huo.

Akizindua kituo hicho kwa Kanda ya Kaskazini kaimu mkuu wa wilaya ya Kibaha Moses Magogwa ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kuwa uwekezaji kwa vijana kutasaidia kuwa na timu bora za baadaye.

Magogwa ambaye ni katibu tawala wa wilaya (DAS) na mwenyekiti wa kamati ya michezo wa wilaya alisema kuwa serikali inaunga mkono suala la michezo kwani ni sehemu ya kutoa ajira kwa vijana.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Pwani Robert Munisi alisema kuwa malengo ya kuanzisha kituo hicho na vingine kwenye kila wilaya itakuwa na vituo vitatu ambapo kutakuwa na vituo 21 kwa mkoa mzima ni kuibua vipaji na kuviendeleza.

Naye mratibu wa kituo hicho Abdulakarimu Alawi alisema kuwa jumla ya vijana 500 wa shule za msingi na sekondari ambapo vijana wanacheza kutegemeana na umri wao.

No comments:

Post a Comment