Serikali imeidhinisha bajeti ya bilioni 24 kwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma General Hospital kwa mwaka wa fedha 2023/24 kuboresha huduma za afya na kufikisha asilimia 99 za utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.
Akizungumza leo jijini Dodoma, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Dkt. Ernest Ibenzi amesema watumishi wa hospitali hiyo wanaendelea kupata mafunzo sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Dkt. Ibenzi amesema mafunzo hayo yanawasaidia kujua teknolojia mpya ili kuendeleza juhudi za kuboresha huduma hospitalini hapo.
Amesema hospital hiyo imekua ikipokea wagonjwa wengi kwa siku wa kufikia na kuondoka takribani 1500 huku wanaolazwa wakiwa 250 hadi 350 akisema hospitali hiyo imekua ikipokea wagonjwa kwa asilimia kubwa na siyo watu wa kutembelea.
Amesema hospitali inajumla ya majengo 12 ya vyumba vya kufanyia upasuaji huku ikipokea wagonjwa70 kwa siku wanaofanyiwa upasuaji kwa lengo la Kuboresha huduma za Afya ndani ya hospitali na kuondoa kero ya ucheleweshwaji wa huduma kwa wananchi.
Dkt. Ibenzi ametoawito kwa Wanawake wajawazito waliofikia hatua za mwisho za kujifungua kuwahi katika vituo vya afya ili kuepusha madhara yatakayoweza kujitokeza na kuepusha vifo vitokanavyo na uzazi.
Kuhusu changamoto ya msongamano wa wagonjwa kwenye wodi ya watoto ambapo watoto hulazwa wawiliwawili katika kila kitanda, Dkt. Ibenzi ameeleza kwamba tatizo hilo litakwisha ndani ya wiki mbili zijazo.
Aidha, Daktari huyo amearifu kwamba hospitali yao inaendelea kutatua changamoto mbalimbali ili wananchi wapate huduma bora.
Kwa miaka miwili iliyopita Hospitali hiyo ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma ilikua ya kwanza kidunia kwa kutoa huduma Nzuri za upasuaji kwa wagonjwa na kupona haraka na kwa wakati.
Akitaja Vipaumbele Dkt. Ibenzi amesema kwa miaka miwili ijayo hospitali hiyo itajenga jengo lingine la gorofa 5 kwa lengo la kuimarisha huduma za Afya kuwa bora zaidi.
Hospitali hiyo inafikisha miaka 103 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1920 ikitekeleza kauli mbiu ya Wizara ya kwamba Huduma bora kipaumbele chetu karibu tukuhudumie
No comments:
Post a Comment