Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na Katibu Tawala wa Wilaya (DAS) Kibaha Moses Magogwa alipokuwa akikabidhi ubingwa kwa timu ya Umwelani iliposhindwa kwa kuifunga Wapolo kwa penati 3-1 kwenye michuano ya Micho Cup kwenye uwanja wa Mwendapole ambapo ilijinyakulia kiasi cha shilingi milioni mbili.
Magogwa alisema kuwa michezo ni kiwanda cha ajira ambayo inaajiri vijana wengi ambapo inapaswa kuwekewa mazingira mazuri ili ajira hiyo iendelee kutoa ajira.
"Tutahakikisha halmashauri zote mbili ya Kibaha Mjini na Wilaya ya Kibaha zinaboresha masuala ya michezo kwani nimeona hamasa kubwa iliyopo kwenye michezo tumeona vijana walivyoshiriki michezo,"alisema Magogwa.
Aidha alise kuwa baada ya timu hiyo kushinda itafika ofisini kwa mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kupongezwa kutokana na ushindi huo kwani Mkuu huyo wa Wilaya ndiye aliyepaswa kuwa mgeni rasmi lakini alipata dharura.
"Dc Nickson John anawapongeza kwa kutwaa ubingwa na amewakaribisha muende ofisini kwake akawapongeze kwani naye ni mdau wa michezo na anafurahi kuona vijana wakicheza michezo,"alisema Magogwa.
Aliongeza kuwa changamoto walizomweleza atazifanyia kazi kwani yeye ni mwenyekiti wa kamati ya michezo ya Wilaya atashirikiana na vyama vya michezo ili kuendeleza jitihada za michezo.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Wilaya ya Kibaha (KIBAFA) Robert Munis alisema kuwa mpango wa chama ni kuwa ni vituo nane vya kuendeleza soka la vijana.
Munis alisema wanapongeza waandaaji ya mashindano hayo kwani ni sehemu ya mpango wa chama kuwa na mashindano mara kwa mara ili kupata timu bora zitakazoshiriki kwenye ligi za Wilaya.
Kwa upande wa mratibu wa michuano hiyo ya Micho Cup Othamn Shija "Micho" alisema kuwa jumla ya timu 24 zilichuana kwenye awamu ya pili ya mashindano hayo.
Shija alisema kuwa changamoto kubwa ni kukosa wafadhili wa kudhamini mashindano hayo ambayo yana lengo la kuibua vipaji na kuwahamasisha vijana kushiriki michezo badala ya kujiingiza kwenye vitendo viovu pia kukuza soka la Kibaha.
No comments:
Post a Comment