John Gagarini, Kibaha
JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Frowin Peter
Mbwale (26) mkazi wa Kawe Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuwa ua kwa
kuwachinja mkewe Oliver Erasto (23) na mtoto wake Emanuel Frowin (3) kutokana
na wivu wa mapenzi.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa waandishi wa habari
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Bonaventura Mushongi alisema kuwa tukio hilo
lilitokea majira ya saa 10:30 usiku eneo la Zinga kata ya Dunda Tarafa ya
Mwambao wilayani Bagamoyo.
Mushongi alisema kuwa katika hali isiyo kuwa ya kawaida juzi siku
ya tukio mtuhumiwa akiwa na mwenzake alijulikana kwa jina la Rajabu Juma (20)
Mkazi wa Makongo Jijini Dar es Salaam waliwaua watu hao kwenye vichaka
vilivyopo kwenye eneo hilo la Kaole.
“Muda huo mtuhumiwa akiwa na mwenzake alimhadaa mke wake kuwa
waende kwenye nyumba yao ambayo inaendelea kujengwa kwa lengo la kuitazama
ambapo mke wake alikubali na kumbeba na mtoto wao na kwenda huko ambako
aliwachinja shingoni,” alisema Kamanda Mushongi.
Alisema kuwa mtuhumiwa kumbe lengo lake halikuwa kuangalia
ujenzi wa nyumba yao huko Kaole kumbe alikuwa na lengo lingine la kufanya
unyama huo ambao aliutekeleza akiwa na rafiki yake huyo ambaye walishirikiana
kumchinja mke na mtoto wake.
“Chanzo cha mauaji hayo ni mtuhumiwa huyo alikuwa akimtuhumu
mume wake kuwa ana uhusiano na mwanaume mwingine aitwaye Hamza mkazi wa Kawe
Jijini Dar es Salaam na kusababisha mauaji hayo ya kusikitisha ambayo
yamewaumiza watu wengi,” alisema Mushongi.
Alibainisha kuwa miili ya marehemu hao ilikutwa ikiwa
imechinjwa na watu hao umbali wa mita 100 kutoka barabara ya magari itokayo
Kaole kwenda eneo la Mbegani.
Aidha alisema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa majira ya saa
3:30 usiku baada ya wananchi Zinga kuwatilia mashaka walipokuwa wakijaribu
kutaka kutoroka na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara upelelezi
utakapokamilika, miili ya marehemu imehifadhiw akwenye Hospitali ya wilaya ya
Bagamoyo kusubiri ndugu kwa ajaili ya mazishi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment