Na John Gagarini, Kibaha
KATIKA kukabiliana na changamoto za
elimu wilaya ya Kibaha mkoani Pwani imetenga bajeti ya
shilingi bilioni 1,789,828,891 kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa shule za
sekondari kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya
Kibaha Halima Kihemba na kusema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kupunguza
changamoto mbalimbali kwenye shule za sekondari wilayani humo.
Kihemba amesema kuwa kabla ya bajeti
hiyo kupitishwa jumlaya shilingi milioni 640,424,679 zimetumika kwa ajili ya
ujenzi wa bweni katika shule za sekondari za Zogowale na Hosteli ya shule ya
sekondari ya Pangani.
Amesema kuwa pia fedha hizo
zimetumika katika ujenzi wa matundu 20 ya vyoo, madarasa matano na nyumba moja
ya mwalimu katika shule za sekondari za Pangani, Simbani na Ruvu Station.
Akizungumzia upande wa shule za
msingi amesema kuwa katika bajeti hiyo zimetengwa kiasi cha shilingi milioni
943,144,394 kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa elimu ya msingi.
Aidha amesema kuwa katika bajeti ya
mwaka wa fedha ya 2015/ 2016 wilaya ilipokea kiasi cha shilingi milioni
140,254, 154 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya mwalimu Kumba, vyumba 9 vya vya
madarasa katika shule za Visiga, Lumumba, Bamba na Matuga.
Amebainisha kuwa fedha hizo pia zimetumika
kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo na ununuzi wa madawati 46, meza 4 na
viti 6 kwa ajili ya shule ya Msingi ya Matuga.
No comments:
Post a Comment