WILAYA ya Kibaha mkoani Pwani imefanikiwa kukamata madawa ya kulevya yenye uzito wa kilogramu 441.6 katika kipindi cha mwaka 2015 / 2016.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Kibaha ambaye pia ni wenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya amesema kuwa katika mapambano dhidi ya madawa ya kulevya kipindi cha mwaka 2015/ 2016 wamefanikiwa kukamata dawa zenye uzito wa kilogramu 441.65.
Kihemba amesema kuwa kati ya hizo Cocain na Heroin ni kilo 6.1, Bhangi kilo 418,mirungi kilo 17.5 ambapo jumla ya kesi 153 zimefunguliwa kwenye kituo cha Polisi cha wilaya ya Kibaha.
Amesema kuwa kesi zilizopelekwa mahakamani ni 132 na zilizo kwenye upelelezi ni 21 ambapo kesi za Bhangi na Mirungi zilizo kwisha mahakamani ni 57.
aidha amesema kuwa jumla ya watuhumiwa ambao walikamatwa na bangi na mirungi ni 163 wanawake wakiwa ni 28 na wanaume ni 135 na wilaya inaendelea kutoa elimu ili watu waepukane na dawa za kulevya.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment