Thursday, May 5, 2016

MADIWANI WATAKA UDHIBITI WA MAPATO UPOTEVU BILIONI 1.1 KWA MWAKA

Na John Gagarini, Kibaha
MADIWANI wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani wameitaka Halmashauri kudhibiti upotevu wa fedha kiasi cha bilioni 1.1 kwa mwaka kutokana makusanyo kuwa chini hivyo kushindwa kufikia malengo.
Wakizungumza kwenye baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo baadhi ya madiwani walisema kuwa kuna upotevu wa fedha nyingi ambapo endapo mianya hiyo ya kupotea fedha itazibwa itasaidia kudhibiti hali hiyo.
Akizungumzia namna fedha hizo zinavyopotea Diwani wa Kata ya Tumbi Hemed Chanyika alisema kuwa wao kama madiwani walifanya utafiti kwenye vyanzo vya mapato na kugundua mapungufu makubwa katika ukusanyaji.
Chanyika alisema mfano ni mapato ya ushuru wa mchanga ambako waligundua kuwa magari yanayoingia kuchukua machanga kwa siku ni magari 103 ambapo gari moja linalipia kiasi cha shilingi 3,000 kwa mwaka mapato ni bilioni 1.1 lakini makiso yaliyowekwa ni milioni 264.6 kwa mwaka tofauti ya milioni 900.
Alisema kwa upande wa stendi  ya Maili Moja makisio yalikuwa ni shilingi milioni 320 kwa mwaka ambapo magari yanayopita ni zaidi ya magari 500 kwa siku ni milioni 503 hadi 564 kwa mwezi ambapo upotevu ni kiasi cha shilingi milioni 183.6 huku Machinjio yakikadiriwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 25 na kufanya upotevu kuwa milioni 56 ambapo kwa siku wanachinjwa ngombe 45 ushuru ukiwa ni shilingi 5,000 kwa mwaka 25.
“Upotevu huu wa fedha ni mkubwa sana hivyo kuna haja ya Halmashauri kujipanga ili kudhibiti hali hii kwnai endapo hali itaendelea hivi hatutaweza kufikia malengo ambayo tumejiwekea kwa mwaka,” alisema Chanyika.
Kwa upande wake Addhu Mkomambo alisema kuwa kwa sasa makusanyo yamefikia asilimia 54 ambapo ilipaswa kuwa yamefikia asilimia 75 kwa kipindi hichi cha robo mwaka wa bajeti.
Mkomambo alisema kuwa kwa miaka mitatu mfululizo Halmashauri ilikuwa ikifikia malengo lakini kwa mwaka huu ni tofauti ambapo ili kuziba pengo hilo inapaswa kufanyike operesheni maalumu kukusanya mapato ili kufikia lengo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Leonard Mlowe Halmashauri alisema kuwa katika kuhakikisha makusanyo hayo yanafikia asilimia 100 atakuwa akikutana na watendaji wa serikeli za mitaa na kata kujadili namna ya kukusanya mapato hayo.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Leah Lwanji alisema kuwa suala hilo watalifanyia kazi kwa kulirudisha kamati ya fedha kwa ajili ya namna ya kudhibiti upotevu wa fedha hizo ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa.
Mwisho.   

No comments:

Post a Comment