Mwandishi
Wetu, Kibaha
JESHI la
polisi mkoani Pwani linawashikilia vijana watatu kwa tuhuma za kumteka
mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Pangani Kata ya Pangani wilayani Kibaha
mkoani Pwani ambaye alikuwaaingie kidato cha pili mwaka huu mwenye umri wa
miaka (16) na kushindwa kwenda shule baada ya kutekwa na vijana watatu kwa
kipindi cha miezi mitatuambapo alipata mimba na vijana hao waliitoa.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwao Kidimu wilayani Kibaha huku akibubujikwa na machozi alisema kuwa vijana hao ambao ni wakulima kati yao wawili ni ndugu walimteka kwa kutumia visu vitatu walivyokuwanavyo.
Aliwataja vijana hao ambao anawatuhumu kumfanyia kitendo hicho kuwa ni
Jovinas Oswald , Isaka Joseph na Faida Joseph (22) ambao ni ndugu walimteka Novemba 3 mwaka jana baada ya kumdanganya kuwa anatakiwa kwenda kuchukua mzigo wa ndugu yake.
“Baada ya kwenda kufuata mzigo huo niliwakuta wakiwa na visu vitatu ambapo
kila mmoja alikuwa na kisu na kunipeleka kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi
kusema kuwa hapo ndipo nitakapokuwa naishi na endapo nitajaribu kutoka basi
wataniua,” alisema.
Alisema kuwa kwa kipindi chote hicho walikuwa wakifunga mlango kwa nje kwa
kutumia kufuli kwa nje huku wakiwa wamemhifadhi kwenye kisehemu mithili ya kajeneza kwani juu waliweka miti na pembeni waliweka matofali na juu waliweka godoro huku yeye akiwa chini hali ambayo ilimfanya ashindwe kutoka pia
ikizingatiwa kuwa nyumba hiyo iko mbali na nyumba zingine na kuwa katika
kichaka.
“Faida ambaye ndiye aliyenifanya kama mke wake alinipa mimba lakini baada
ya kuona hivyo walinilazimisha kuitoa kwa kutumia majani ya chai ambayo
yalichemshwa na maji na kuniamuru ninywe na kusababisha mimba kutoka ambapo nilitokwa na damu nyingi na kupata maumivu makali,” alisema mwanafunzi huyo.
Aidha alisema kuwa walimtengenezea kajumba kadogo kwa kupanga matofali na
miti kisha yeye kuingia humo mfano wa kaburi ambapo alikuwa akijisaidia
kwenye mifuko ya plastiki na chupa kwa ajili ya haja ndogo na kuoga ni humo
ndani.
“Kwa upande wa chakula walikuwa wakipika usiku tu kwani walikuwa wakifika
majira ya saa sita au saba usiku wanapika tunakula ila asubuhi na mchana
nilikuwa sili chakula hata mavazi yangu waliyachoama moto nikawa navaa nguo
ya moja ya vijana hao,” aliongeza.
Aliongeza kuwa siku moja vijana hao walisahau kufunga mlango na ndipo
alipotoka na kuomba msaada kwa mtu ambaye alimpeleka hadi nyumbani kwa
walezi wake ambao ni babu na bibi yake ambao ndiyo waliokuwa wakiishi naye
kwa muda wote.
Kwa upande wake babu wa mwanafunzi huyo Daud Zakayo alisema kuwa mwanafunzi
huyo alitoweka katika mazingira ya kutatanisha na walifanya jitihada
kumtafuta ambapo walitoa taarifa polisi na kwa ndugu lakini bila ya
mafanikio.
Zakayo alisema kuwa baada ya mjukuu wao kupatikana walitoa taarifa polisi
ambapo vijana hao walikamatwa kwa ajili ya mahojiano kuhusiana na tukio
hilo.

Naye mwalimu
wa shule aliyokuwa akisoma Peter Mihayo alisema kuwa mwanafunzi huyo
hajafukuzwa ila atasubiri hadi suala lake litakapokamilika kwani tayari liko
kwenye vyombo vya sheria.
Kamanda wa
Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alipoulizwa kuhusiana na
tukio hilo alisema kuwa watuhumiwa wanashikiliwa na mara upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment