Na John Gagarini, Kibaha
MWENYEKITI wa Klabu ya Simba Ismail Aden Rage ameendesha
harambee kuchangia tawi la Simba Kwa Mfipa wilayani Kibaha mkoani Pwani kwa
ajili ya shughuli mbalimbali ambapo alifanikisha kupatikana kwa kiasi cha
shilingi 420,000.
Harambee hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki Kwa Mathias wilayani
Kibaha kwenye ukumbi wa Back Yard ambapo mbali ya kuendesha harambee walijadili
mambo mbali mbali ya kuisaidia klabu hiyo kufanikiwa kwenye mashindano
mbalimbali.
Rage alitoa kiasi cha shilingi 100,000 ikiwa ishara ya
kuanzisha harambee hiyo na kufuatiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Taifa NEC kutokea wilayani Kibaha Rugemalila Rutatina ambaye
alitoa kiasi cha shilingi 100,000.
Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry
Koka yeye aliahidi kutoa kutoa kiasi cha shilingi 100,000 na wanachama, wapenzi
na mashabiki wa timu hiyo nao walichangia fedha na kufikia kiasi hicho.
“Fedha hizi zilizochangwa zinapaswa kutumika kwa ajili ya
malengo yaliyowekwa ikiwa ni pamoja na kufungua akaunti pamoja na mambo
mbalimbali ya tawi,” alisema Rage.
Aliwataka wadau wa Simba kujitokeza kuisaidia timu yao ili
kuhakikisha inafanikiwa kutetea ubingwa wake wa ligi kuu ya Voda Com ambao kwa
sasa inaonekana kama imeuweka rehani baada ya kufungwa na Mtibwa Sugar ya
Morogoro.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment