Na Mwandishi Wetu,
Kibaha
MWILI wa
mfanyabiashara wa Jijini Dar es Salaam Ambrose Mapunda anayekadiriwa kuwa na
umri kati (50) na (55) umekutwa chini ya uvungu wa nyumba ya kualala wageni
huku ukiwa mtupu bila ya nguo.
Akizungumza na
waandishi wa habari kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ofisa
upelelezi wa mkoa wa Pwani wa jeshi la polisi Juma Yusuph alisema kuwa tukio
hilo lilitokea kwenye nyumba ya kulala wageni kwenye nyumba ya kulala wageni ya
Cham Cham iliyopo wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Alisema tukio
hilo lilitokea kati ya Fabruari 22 na 24 kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni huku
ukiwa na jeraha kubwa kichwani huku shingo yake ikiwa imenyongwa.
“Marehemu alikutwa
akiwa chini ya uvungu huku mwili wake ukiwa hauna nguo na jeraha huku ukiwa
umenyongwa shingo ambapo mtu aliyehusika na tukio hilo hakuweza kufahamika mara
moja,” alisema kamanda Yusuph.
Alibainisha
kuwa marehemu hakukutwa na kitu chochote licha ya kuwa alifika kwenye nyumba
hiyo ya kulala wageni akiwa na begi kwenye chumba namba mbili.
“Ujumbe
uliokutwa kwenye chumba hicho ulisema kuwa umenidhulumu tulikubaliana unilipe
kiasi cha shilingi 20,000 lakini hujanilipa, ujumbe huu umeandaikwa na mtu
asiyefahamika,” alisema Kamanda Yusuph.
Aidha alisema
kuwa mhuduma na mlinzi wa nyumba hiyo ya kulala wageni wanashikiliwa kwa
mahojiano zaidi kuhusu tukio hilo na polisi wanaendelea na uchunguzi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment