Na John Gagarini, Bagamoyo
UBALOZI wa Misri nchini
umetoa msaada ya vifaa mbalimbali vya kisasa katika hospitali ya wilaya ya
Bagamoyo mkoa wa Pwani vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja.
Vifaa hivyo vilivyotolewa ni
Madawa, Vitanda pamoja na vya wodi ya upasuaji kwa ajili ya kuboresha hudum za
afya kwenye hospitali hiyo.
Akikabidhi vifaa hivyo balozi wa Misri hapa nchini Bw Hossam
Eldin Moharam alisema wananchi wa Misri wameamua kutoa msaada huo
kwa marafiki zao wa Bagamoyo ili kudumisha na kuenzi urafiki wa muda
mrefu baina ya wananchi wa nchi hizo mbili.
Bw Moharam alisema kuwa hapendi kuita ni msaada wa
vifaa walivyovitoa kutokana na ukaribu na urafiki uliopo baina ya nchi
hizo.
“Tunaomba vifaa hivi vilivyotolewa kwenye hospitali
hii vilindwe kwani vinahitaji uangalizi mkubwa ili viweze kusadia kutoa huduma
bora za afya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo Bw Shukuru Mbatto alisema msaada huo ni chachu kwa watumishi wa hospitali hiyo katika uboreshaji wa utoaji huduma bora .
Naye mmoja wa wadau waliofanikisha upatikanaji wa msaada huo, Bw Yusuph Kikwete alisema akiwa ni kiongozi wa muungano wa marafiki wa Bagamoyo walizungumza na balozi huyo kuhusiana na ombi la msaada wa vifaa kwa ajili ya maabara mpya ya hospitali hiyo .
Mwisho
No comments:
Post a Comment