Na
Mwandishi Wetu, Kibaha
MWANAFUNZI
wa darasa la kwanza wa shule ya Msingi Mbaya, Geuza Patrick (12) amekufa
kwa kujinyonga kwa kamba ya katani.
Kwa
mujibu wa kaimu kamanda wa Polisi mkoani Pwani Gregory Mushi alisema kuwa tukio
hilo lilitokea Februari 13 mwaka huu majira ya saa 12 jioni huko kitongoji cha
Msufini tarafa ya Chalinze wilayani Bagamoyo.
Kamanda
Mushi alisema kuwa mwanafunzi huyo alijinyonga kwenye Mti wa Mwembe nyumbani
kwao.
Alisema
kuwa chanzo cha kujinyonga bado hakijafahamika na polisi wanaendelea na
uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
Aidha
alisema mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.
Mwisho.
Na
Mwandishi Wetu, Kibaha
SHULE
ya Sekondari ya Bundikani ya Kata ya Maili Moja wilayani Kibaha imeanza
kuchukua hatua kali kwa wanafunzi wanaovaa suruali za kubana maarufu kama modo
kwa kuzichana.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi mjini Kibaha mwalimu mkuu wa shule hiyo Flora
Chibululu alisema kuwa juzi walichana suruali za wanafunzi watatu kutokana na
kwenda shuleni na suruali hizo kinyume cha sheria.
Alisema
kuwa baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamekuwa na tabia ya kuzirekebisha
kwa kuzibana suruali hizo licha ya kuwa zinashonwa kawaida na kukiuka taratibu
za shule.
“Suruali
hizo za shule hushonwa vizuri lakini wao huzipeleka kwa fundi na kuzibana sawa
na miili yao maarufu kama modo, tulishawapiga marufuku kuzibadili nguo hizo
lakini wanakaidi hali iliyotufanya tuchukue hatua hiyo ili kuleta nidhamu
shuleni,” alisema Chibululu.
Chibululu
alisema kuwa baadhi ya wanafunzi wamekuwa wakikiuka taratibu za shuleni na
kuiga tabia ambazo zinashusha taaluma hivyo shule itakabiliana na vitendo
kinyume cha taratibu za shule.
Aidha
alisema wataendelea kuzichana suruali hizo kwa mwanafunzi atakaye vaa kinyume
cha sheria za shule kwani huo ni utovu wa nidhamu na lazima wanafunzi wafuate
taratibu za shule.
Mwisho.
Na
Mwanidshi Wetu, Kibaha
WAFANYABIASHARA
kwenye kata ya Maili Moja wilayani Kibaha mkoani Pwani wametakiwa kupima afya
zao kwa mujibu wa sheria ili waweze kuhudumia wateja wao wakiwa na afya njema
vinginevyo watapelekwa mahakamani kwa kukiuka kanuni za afya.
Hayo
yalisemwa na ofisa afya wa kata hiyo Ally Shah, wakati akizungumza na waandishi
wa habari ofisini kwake mjini Kibaha na kusema kuwa watakaokataa kupima afya
zao watapelekwa mahakamani.
Shah
alisema kuwa hivi karibuni baadhi ya wafanyabiashara waligoma kwenda kupima
afya zao wakidai kuwa kiwango cha kupima ni shilingi 5,000 ambayo ilipangwa na
halmashauri wakidai kuwa ni kubwa.
“Wafanyabiashara
wanatakiwa kupima afya ili kutoa huduma wakiwa na afya njema ili kuepuka
maambukizi ya magonjwa mbalimbali kama vile kifua kikuu na magonjwa ambayo
yanaambukiza kwa haraka,” alisema Shah.
Alisema
kuwa baadhi ya wafanyabiashara hao wamekuwa na hofu ya kupima afya kuwa
wataonekana na maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI jambo ambalo alisema kuwa
upimaji huo hauhusiani na kupima vipimo vya ugonjwa huo.
“Wasihofie
kupima afya kwani magonjwa yanayopimwa hayahusiani na ugonjwa wa UKIMWI na kama
mtu anataka kupima ugonjwa huo ni hiyari yake mwenyewe na si kwa lazima kama sheria
inavyoelekeza,” alisema Shah.
Aidha
alisema kuwa magonjwa yanayopimwa ni pamoja na magonjwa ya zinaa, kifua kikuu
na haja kubwa hivyo wafanyabiashara wapime afya zao kwani ni kwa faida yao na
wateja wanaowahudumia.
Katika
hatua nyingine alisema kwa sasa wanaendelea na kuboresha usafi wa mazingira
ambapo vimeundwa vikundi mbalimbali vya usafi kwa ajili ya kuhakikisha
mazingira ya Mji wa Kibaha ambapo sheria ndogondogo ya halmashauri inawatoza
kiasi cha shilingi 50,000 kwa mtu atakayechafua mazingira.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment