Sunday, October 18, 2026

KIDULI FC YAICHABANGA DRAGON FC 2-0

TIMU ya soka ya Kiduli Fc imeichapa timu ya Dragon Fc kwa bao 2-0 kwenye mchezo wa ligi daraj la tatu Wilaya ya Kibaha mchezo uliofanyika uwanja wa Mwendapole Kibaha.

Hadi mapumziko timu hizo zilikuwa hazijafungana bao lolote ambapo kila timu ilifanya mabadiliko ya wachezaji ambayo yaliisaidia Kiduli Fc.

Kiduli Fc iliandika mabao yake kupitia kwa Shauri Schone dakika ya 21 huku bao la pili likifungwa na Isihaka Mohamed dakika ya 25.

No comments:

Post a Comment