
WAZIRI wa Katiba na Sheria Abdala Ulega amewataka wananchi kujitokeza kupata huduma za Msaada wa Kisheria kutoka kwa wataalam wa sheria.
Ameyasema hayo stendi ya zamani ya Maili Moja Kibaha wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia awamu ya pili kwa Mkoa wa Pwani.
Ulega amesema Msaada wa kisheria ni kwa watu wote bila ya kujali uwezo wa mtu na unatolewa bure hasa kwa makundi yakiwemo ya wanawake watoto watu wenye ulemavu na wale wasio na uwezo.
No comments:
Post a Comment