Tuesday, October 13, 2026

MADEREVA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI WAKATI WOTE.


Madereva wametakiwa kuzingatia sheria na taratibu za usalama barabarani wakati wote wanapotumia barabara, badala ya kuzifuata pale wanapomuona askari wa usalama barabarani.

Wito huo umetolewa Oktoba 13, 2026, na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Edson Mwakihaba, wakati akizungumza katika kipindi maalumu cha elimu ya usalama barabarani kilichorushwa na kituo kimoja cha redio wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

Mwakihaba ameeleza kuwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani litaendelea kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa wananchi wanatumia barabara kwa usalama na kufika salama katika safari zao.

Aidha, amewataka madereva wote wa vyombo vya moto kuhakikisha wanamiliki leseni halali za udereva na kupata mafunzo katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali, badala ya kujiunga na vyuo ambavyo vimefungiwa au havitambuliki kisheria.

Amesisitiza kuwa uzingatiaji wa sheria za usalama barabarani ni wajibu wa kila mtumiaji wa barabara na unapaswa kuzingatiwa wakati wote ili kupunguza ajali na kulinda maisha ya wananchi.

No comments:

Post a Comment