Friday, October 2, 2026

DC NKURLU AOMBA USHIRIKIANO

MKUU wa Wilaya mpya ya Kibaha Fadhil Nkurlu amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Nickson John nakuomba ushirikiano kwa viongozi ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Makabidhiano hayo yalifanyika Mjini Kibaha mbele ya wakuu wa vitengo na idara za Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha ambapo Nkurlu alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Songwe huku John akihamishiwa Wilaya ya Songwe na Makabidhiano ya wakurugenzi Warda Maulid anayehamia Manispaa ya Kibaha na Dr Rogers Shemwalekwa aliyekuwa Mkurugenzi.

Nkurlu amesema kuwa anaomba ushirikiano kutoka kwa viongozi na wadau ili kuleta maendeleo kwani ameletwa kwa ajili ya kutumikia wananchi.

Naye Mkuu wa Wilaya Songwe John amesema kuwa kwa ushirikiano na Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha makusanyo yameongezeka kutoka bilioni 11 hadi bilioni 39.

John amesema kuwa mradi mwingine ni wa maegesho ya magari makubwa ambayo inauwezo ya kuegesha magari 3,000 na ujenzi wa Kongani za viwanda zenye uwezo wa kutoa ajira kwa watu 200,000.

Kwa upande wake Mkurugenzi aliyepita Dk Rogers Shemwelekwa amesema kuwa anashukuru kwa ushirikiano aliyopewa na madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.

Naye Mkurugenzi mpya Warda Maulid amesema kuwa anamshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumpangia Halmashauri ya Kibaha akitokea Simanjiro kama Katibu Tawala.

Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka amesema kuwa watatoa ushirikiano kwa viongozi hao waliohamishiwa kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha.


No comments:

Post a Comment