Hayo yalisemwa na NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kwenye ofisi za Halmashauri hiyo zilizopo Mlandizi.
Alisema kuwa serikali inafanya shughuli zake kimkakati hivyo lazima nao wafanye kazi kwa kuzingatia mikakati hiyo ya serikali ili mipango ya maendeleo kwa wananchi ifikiwe.
"Serikali ina mikakati yake hivyo lazima kila mtumishi wa umma ahakikishe anazingatia mikakati iliyopo ili kufanikisha malengo ya maendeleo kwa wananchi ambapo wanawategemea watumishi kuwaonyesha njia,"alisema Kikwete.
Alisema asingependa kuona watumishi hawawajibiki kwenye maeneo yao ya kazi na kusababisha malengo ya kuwaletea maendeleo wananchi yasifanikiwe hivyo wasije wakajikuta wanaondolewa au kufukuzwa kazi.
"Kutokana na changamoto zilizopo hapa ofisa utumishi Edward Mahona nakutaka ushughulikie chanfamoto za watumishi siyo lazima kuleta kwetu kwani baadhi ya mambo mnaweza kuyatatua wenyewe hivyo tatua mara moja,"alisema Riziwani.
Aidha alisema kuwa ofisa huyo anatakiwa kukaa na watumishi na kuongea nao kujua changamoto zao kwani malalamiko yaliyotolewa yanapaswa kufanyiwa kazi ili wafanye kazi kwa moyo kwani shida zao zinatatuliwa.
Moja ya watumishi Winifrida Toegale ambaye ni ofisa mtendaji wa kijiji alisema kuwa wanatumia fedha zao binafsi kwani hakuna fedha wanazopewa kwa ajili ya kuendeshea ofisi.
Toegale alisema kuwa licha ya kutumia fedha zao za mishahara lakini kwa upande wao walioajiriwa mwaka 2012 hawakupandishwa vyeo hadi mwaka 2020 jambo ambalo limekuwa changamoto kubwa na inawavunja moyo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha Butamo Ndalahwa alisema kuwa wanakabiliwa na uhaba wa watumishi 441 ambapo waliopo ni 1,571 na mahitaji ni 2,012 na wameweka bajeti ya kuajiri watumishi 211 kwenye kada mbalimbali.
Ndalahwa alisema kuwa madai ya watumishi 342 ni milioni 756 ambapo madai yaliyolipwa ni 251 ya shilingi milioni 455 bado madai 91 yenye thamani ya shilingi milioni 329 kwa upande wa watumishi 70 waliogushi vyeti 56 walijaza fomu huku 12 bado taratibu zinaendelea.
No comments:
Post a Comment