RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri jeshi mkuu Mhe, Dkt,Samia Suluhu Hasani anatarajiwa kuwa mgeni rasmi Katika maadhimisho ya Miaka 60 ya Jeshi la kujenga Taifa JKT.
Kauli hiyo imetolewa na waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga Taifa Mhe, Innocent Bashungwa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.
Mhe, Bashungwa amesema kilele Cha maadhimisho ya Miaka 60 ya JKT kinatarajiwa kuadhimishwa rasmi julay 10 2023 Katika viwanja vya Jamuhuri jijini Dodoma ambapo wageni mbalimbali watashiriki kutoka ndani na nje ya Nchi.
Aidha amewaalika viongozi wote wa serikali, taasisi mbalimbali za umma na binafsi,watumishi,wananchi wa mkoa wa Dodoma na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kuhudhuria siku ya kilele Cha maadhimisho Hayo.
Hata hivyo Maadhimisho Hayo yanatarajiwa kuanza saa kumi na Mbili Asubuhi ambapo kutakuwa na maonyesho ya vifaa mbalimbali vya SUMA JKT, burudani za ngoma kutoka vikundi vya JKT na wasanii Mbalimbali.
No comments:
Post a Comment