NAIBU Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omar Kipanga amewataka wananchi wa Mafia wanaomiliki mashamba na viwanja vilivyopo karibu na ufukwe wa bahari kutokuyauza maeneo yao badala yake waingie ubia.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo kwenye Kata ya kirongwe Vijiji vya Banja na Jojo.
Kipanga alisema kuwa baadhi ya wananchi wa Mafia wamekuwa wakiuza maeneo yao kwa wanaowaita wawekezaji ambao wanavutiwa na maeneo hayo.
"Wananchi wanapaswa kuyakodisha maeneo hayo au wangie mikataba kwa kugawana asilimia angalau nusu kwa nusu ili kupata faida zaidi kuliko kuyauza,"alisema Kipanga.
Alisema kuwa mashamba/viwanja ni vyao lakini kwa Sasa utaratibu mzuri wa kupata maendeleo ya ardhi yako sio kuuza bali ni kuingia ubia na wawekezaji.
"Acheni kabisa tabia hii siyo nzuri itafika hatua ardhi yote ya maeneo ya Pwani ya Mafia itakuwa inamilikiwa na wageni na wenyeji watakua hawana ardhi wakati ni sasa kila mmoja apate faida ya ardhi katika uwekezaji,"alisema Kipanga.
Aidha alisema kuwa Serikali ya Rais Samia na Chama Cha Mapinduzi (CCM) inaboresha barabara za Mafia ni wazi maeneo hayo yanaenda kupanda thamani hivyo ni muhimu kuwawekea na kizazi cha baadae kupitia makubaliano kwenye ardhi.
No comments:
Post a Comment