MFUKO wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) umeleta mabadiliko makubwa kwa walengwa wake ambapo Zubeda Juma miaka (70) mkazi wa Kijiji cha Kisanga kata ya Masaki Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani amefanikiwa kujenga nyumba ya tofali kutoka nyumba ya udongo aliyokuwa anaishi awali.
Aidha Halima Salehe naye amefanikiwa kujenga nyumba ya tofali kutokana na fedha za mfuko huo ambao umekuwa mkombozi kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini.
Juma akitoa ushuhuda mbele ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete alipotembelea Kijiji hicho kuzungumza na walengwa na wananchi.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ridhiwani Kikwete alimchangia na wadau wengine walimchangia huku Halmashauri ya Kisarawe ikiahidi kuhakikisha inakamilisha sehemu itakayobakia.
Alisema kuwa nyumba yake ambayo ni ya kisasa imekamilika ambapo anaishi ila amebakiza kuweka milango na madirisha ambayo ameyaziba kwa kutumia mabati.
Naye Salehe alisema kuwa nyumba yake imefikia hatua ya boma ili kukamilika na kumshukuru Rais Dk Samii Suluhu Hassan kwa kuendeleza mpango huo kutoka kwa mtangulizi wake na kuwafanikisha kubadilisha maisha yao.
Naibu Waziri Ridhiwani alisema mpango huo una lengo la kuwaondoa wananchi kwenye lindi la umasikini ambapo watu milioni 1.3 wananufaika na mpango huo wa kunusuru kaya maskini na kuondoka kwenye umaskini na utegemezi.
No comments:
Post a Comment