Monday, September 4, 2023

POLISI PWANI WAKAMATA WATUHUMIWA NYAMA YA SWALA NA MAGAMBA 11 YA KAKAKUONA

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na askari wa wanyama pori limefanikiwa kukamata watubuhumiwa 14 wakiwa na nyama ya swala na magamba 11 ya mnyama Kakakuona.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo ACP Muhudhwari Msuya amesema kuwa baadhi ya watuhumiwa walifikishwa mahakamani.

Msuya amesema kuwa kukamatwa watuhumiwa hao 14 ni mafanikio ya jeshi hilo ambapo kati ya hao watuhumiwa watatu wamefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Amesema kuwa watu watatu wamehukumiwa vifungo tofuati kutokana na kukutwa na makosa ya ubakaji na ulawiti.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Salim Issa ambaye amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kulawiti mwingine ni Albino Anthony amehukumiwa kifungo cha miaka 30 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kubaka.

"Mazoea Salum amehukumiwa kifungo cha miaka 30 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kubaka huku Hamisi Idd amehukumiwa kifungo cha miaka 20 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupatikana na nyara za Serikali,"amesema Msuya.

Aidha amesema kuwa Yusuph Athuman naye  amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kupatikana na nyara za Serikali.

"Katika kipindi cha mwezi Agosti jumla ya kesi zilizoshinda mahakamani zilikuwa 75 zikiwemo hizo za watuhumiwa ambao walihukumiwa jela maisha na wengine jela miaka 30 kwa kosa la kulawiti na kubaka watuhumiwa waliotiwa hatiani katika mahakama za Mkoa wa Pwani na kwenda jela kwa baadhi ya kesi,"amesema Msuya.

No comments:

Post a Comment