Thursday, September 28, 2023

SHULE BORA YAWAJENGEA UMAHIRI UFUNDISHAJI SOMO LA HISABATI

KATIKA kuhakikisha wanafunzi wa shule za msingi wanapata uelewa wa somo la hisabati Mkoani Pwani Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia na Taasisi ya Elimu Tanzania kupitia program ya Shule Bora imewapatia mafunzo walimu wa somo hilo.

Akizungumza Wilayani Kisarawe baada ya ufunguzi wa mafunzo kwa viongozi wa elimu kuhusu uboreshaji ufundishaji na ujifunzaji wa umahiri wenye changamoto katika somo la hisabati Ofisa elimu Mkoani humo Sara Mlaki amesema kuwa mafunzo kwa walimu hao yatawajengea uwezo ili kupata mbinu bora za umahiri za ufundishaji wa somo la hisabati.

Aidha mafunzo hayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Taasisi ya Elimu Tanzania kupitia Program ya Shule Bora ambayo inatekelezwa katika mikoa tisa ya Tanzania Bara kwa Ufadhili wa Serikali ya Uingereza na kwa Usimamizi wa Cambridge Education.

Mafunzo hayo yaliendeshwa na  wawezeshaji kutoka vyuo vya Ualimu vya Tukuyu  na Mpwapwa ambapo washiriki wa  mafunzo hayo ni viongozi wa Elimu kutoka katika ngazi ya Mkoa  wakiwemo Walimu, Walimu  wakuu, Maofisa Elimu Kata, Maofisa Elimu Awali na Msingi kutoka katika Halmashauri tisa na shule teule za Wilaya ya Kisarawe.

No comments:

Post a Comment