Tuesday, September 12, 2023

*DKT JAFO AFUNGUA MRADI WA MAJI KITUO CHA AFYA MZENGA*

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa RAIS Muungano na Mazingira Mhe Dkt Selemani Saidi Jafo amefungua Mradi wa Maji katika Kituo Cha Afya Mzenga na kuwataka wananchi kuutunza Mradi huo 12.09.2023.

Akiziungumza wakati wa kufungua Mradi huo wa Maji alisema ni wajibu wa wananchi Hao wa Mzenga kuitunza miundombinu ya Mradi ili uweze kudumu kwa Muda mrefu huku ukiwahudimia wananchi mbalimbali na wale wanaofika Katika kituo cha Afya Mzenga,

*"Ndugu wananchi nimehangaika sehemu mbalimbali kutafuta wafadhili na kuwapata Hawa ndugu zetu Afrika Relief ambao wameweza kutusaidia kutatua hii kero ya maji hapa Mzenga niwashukuru sana Hawa afrika  Relief kukubali kutujengea Mradi Huu mkubwa alisisitiza Mhe Dkt Jafo*"

Nae Meneja wa Taasisi ya Afrika Relief Kanda ya Tanzania Mohamed Gewily alishukuru kisarawe kwa kupokea msaada wa Mradi huo wa Maji huku akitaja umegarimu  Shilingi Milioni Tisa na Laki Tatu na Elfu Hamsini hivyo akatoa wito zaidi kwa Wanakisarawe hasa Mzenga kuitunza miundombinu ya Mradi ili idumu na Kuendelea Kutoa huduma kwa Muda mrefu,

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya kisarawe katika ufunguzi wa mradi wa Maji Ndg Nancy Kasamala Alisisitiza kuhifadhi miundombinu ya Mradi pamoja na Kutoa wito kwa Jamii Kuendelea kuzitumia vyema Kamati za maji za Vijiji katika kusimamia  Mradi,

*"Ndugu zangu tuliopo hapa naomba niwakushe  jambo Moja kuna bodi ya maji Vijijini Hivyo nashauri mshirikiane na Uwongozi wa kituo Cha Afya Mzenga kwa kuendesha Mradi huu ambao umejengwa hapa kituoni badala ya Kijijini alishauri Ndugu Kasamala*"

Mradi Huu wa maji katika Tarafa ya Mzenga kata ya Mzenga Kijiji Cha Mzenga umefadhiliwa na Taasisi ya Afrika Relief umegarimu  dhamani ya Milioni Tisa na Laki Tatu na Elfu Hamsini unategemea kuwahudumia watu Elfu Moja  mia Nne na Sitini na Tatu pamoja watu mbalimbali wanaofika kituo Cha Afya Mzenga,

Aidha Mradi huo pia Unategemea kwa Raia kuchangia Bei ya Maji kwa Ndoo  Moja ya  lita Ishirini kwa  Shilingi Arobaini Tu kwa Mujibu wa muongozo ili uweze kuendesha Miundombinu mbalimbali pamoja na Kukarabati.

No comments:

Post a Comment