Katibu wa Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoa wa Pwani ndugu Omary Abdull Punzi katika Mahafali ya 22 ya Shule ya msingi Kambarage wilaya Kibaha Mkoani Pwani amewambia wazazi,walimu wanafunzi na wageni waliohudhuria mahafali kulinda vitu vyao vikiwemo vilivyoachwa na waasisi wa Taifa letu.
Punzi amesema kuwa wananchi wanawajibu wa kulinda vya kwao na kufanya matendo yaliyo kuwa mema waliorithishwa na wazee pamoja na kuunga nuhudi za Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema kuwa wanapaswa kuwekeza katika idara ya Elimu na maeneo mingine sambamba na hilo aliwaeleza Falsafa mbili za kuwa mzalendo za TA TE TI TO TU na ile ya SA SE SI SO SU Falsafa hizi zinapendwa sana kuzungumzwa na Mheshimiwa Paul Petro Kimiti Mwenyekiti wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Taifa Mhe Kimiti alishika nafasi mbalimbali serikalini.
Katika Mahafali hiyo Mgeni Rasmi alikuwa Ndugu Festo Issingo Meneja wa benki ya NMB Mkoa wa Pwani alichangia madawati 100 baada ya kuambiwa kuna uhaba wa madawati.
Kwa Upande wa Mkuu wa shule ya Msingi KAMBARAGE alimshukuru Katibu wa Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoa wa Pwani na Meneja wa benki ya NMB Mkoa wa Pwani.
Kwa niaba ya wazazi na walimu walimpendekeza ndugu Omary Abdull Punzi Katibu wa Taasisi ya kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa mlezi wa Shule ya Kambarage Nyerere kwa kuwasaidia mawazo ili kufanikisha malengo yao.
No comments:
Post a Comment