JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani limewakamata wahamiaji haramu watatu toka nchi mbalimbali kwa kuingia nchini bila ya kibali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kaimu kamanda wa polisi mkoani Pwani ACP Muhudhwari Msuya imesema kuwa watuhumiwa hao wamekabidhiwa Uhamiaji kwa hatua za kisheria.
Msuya amesema kuwa watuhumiwa hao ni kutoka nchi za Ethiopia mmoja, Kenya mmoja na Uganda mmoja.
Amesema kwenye matukio mengine jeshi hilo limekamata jumla ya Pikipiki 111 za aina mbalimbali Haoujue 23, Boxer 30, Fekon 10, SanLg 16, Sinray 1, Kinglion, Senke 01, bajaji 4 na Tvs 23 mali zidhaniwazo kuwa za wizi na watuhumiwa 97 walikamatwa.
Pia kwenye matukio mengine jeshi limefanikiwa kukamata Bhangi viroba 7, Puli 60, Kete 791 na Mbegu za Bangi kilogramu 5, Mirungi Kilogramu 5, Bunda 3 za mirungi ambapo umla ya watuhumiwa 114 wamekamatwa katika makosa hayo.
No comments:
Post a Comment