BEI ya Vitunguu kwenye Soko la Loliondo Halmashauri ya Manispaa Kibaha iko juu kutoka shilingi 130,000 hadi 250,000 kwa gunia.
Aidha viazi mbatata ambavyo ni maarufu kwa ajili ya kukaangia chipsi vimeshuka bei kutoka shilingi 140,000 hadi 70,000 kwa gunia.
Akizungumza ofisini kwake Mjini Kibaha Naibu Katibu Mkuu wa soko hilo Alex Msimbe alisema kuwa kwa sasa bidhaa nyingi bei zake hazijapanda sana bali bei iko wastani.
Msimbe alisema kuwa bei hiyo ya vitungu imeongezeka sana kutokana na kipindi hichi ndiyo bei huwa inapanda sana lakini baadaye bei hiyo itashuka.
"Bei ya tenga la nyanya imeshuka kutoka kati ya shilingi 85,000 na 70,000 hadi 35,000 huku mchele ukiuzwa kati ya shilingi 3,000, 2,500 hadi 2,700 kwa kilo na maharage yakiuzwa kati ya shilingi 2,700 hadi 3,000 kwa kilo.
Alisema kuwa bei ya unga wa sembe ni kati ya shilingi 1,400 na 1,500 kwa kilo na ngano ni shilingi 125,000 kwa kilo 50 huku sukari ikiuzwa shilingi 3,000 kwa kilo.
"Bei za bidhaa nyingi bei hazijapanda kwani kipindi hichi ni cha baadhi ya maeneo ni mavuno na mengine ndiyo wamepanda muda siyo mrefu hivyo kutoathiri sana bei,"alisema Msimbe.
Aidha alisema kuwa kwa sasa hakuna changamoto kwenye soko hilo kwani miundombinu ikiwemo ya maji, umeme na huduma muhimu kama za vyoo zote ziko vizuri kwani wanashirikiana vizuri na Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha ambao ndiyo wanaowasimamia.
"Kuhusu mitaji baadhi ya wafanyabiashara wananufaika na mikopo ya Halmashauri ile ya asilimia 10 na asilimia 7,"alisema Msimbe.

No comments:
Post a Comment