Sunday, June 28, 2026

MAWAZO VIJANA CHALLENGE KUTUMIKA KIMAENDELEO



SERIKALI imesema kuwa itatumia mawazo ya vijana walioshiriki shindano la Vijana Uchumi Challenge kuwa mpango ambao utaleta suluhisho la namna ya kutatua baadhi ya changamoto ndani ya jamii.

Hayo yalisemwa Kibaha na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Jenifa Omollo wakati wa kufunfa mafunzo ya siku nne kwa vijana 100 walioandika mawazo juu ya masuala ya uchumi kupitia jukwaa la Vijana Uchumi Challenge.

Omollo alisema kuwa mawazo yaliyoandikwa na vijana yameonyesha kuwa yakiboreshwa yanaweza kuwa mpango mzuri ambao unaweza kukabili changamoto mbalimbali ndani ya jamii na Taifa kwa ujumla.

"Mawazo yote yaliyowasilishwa hayataachwa badala yake yataboreshwa na kupatiwa fursa ili yawe mpango ambao utakuwa suluhu kwa baadhi ya changamoto ili kuleta tija na kusaidia Taifa mojawapo likatoa ajira kwa vijana,"alisema Omollo.

Alisema kuwa mawqzo hayo ni bunifu ambazo zimeonyesha jinsi gani vijana walivyokuwa na vipaji ambavyo vitatoa ajira na kuwa na manufaa kwa watu wengi hivyo kulisaidia Taifa.

Naye mwenyekiti wa kamati ya Vijana Uchumi Challenge Joseph Malecela alisema kuwa jumla ya mawazo zaidi ya 7,000 ya vijana kote nchini wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 yaliwasilishwa na kuchujwa na kubaki 100 ambayo yatashindanishwa kupata mshindi.

Malecela alisema kuwa washiriki hao 100 ambao waliiingia kambini kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere wamechujwa na majaji wabobezi wa masuala ya uchumi na fedha na kubaki 10 watashindana ili kumpata mshindi wa shindano hilo.

Rais Dk Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha kumpata kijana mwenye wazo zuri Julai 6 mwaka huu Jjiini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Julius Nyerere Internation Convention Centre (JNICC) Jijuni Dar es Salaam.







mwisho


No comments:

Post a Comment