Thursday, June 25, 2026

MAWAKALA WAITWA KUCHANGAMKIA VIPAJI TUMBI KIBAHA

MAWAKALA wa michezo ikiwemo soka wametakiwa kujitokeza kushuhudia vipaji vya wacehzaji chini ya miaka 17 na 22 kwenye mashindano ya Compassion ili kuwa na timu bora zitakazozalisha wachezaji wakulitumikia Taifa ambapo moja zao la wachezaji hao ni Dickson Job anayechezea timu ya Yanga.

Hayo yamesemwa Mjini Kibaha na Lucas Kiluwasha ambaye ni mwenyekiti wa Mashindano ya Compassion Kanda ya Mashariki kwenye Viwanja vya Shirika la Elimu Kibaha Tumbi.

Mashindano hayo ambayo ni ya nne kufanyika yameweza kuwatoa wachezaji wengi akiwemo Dickson Job wa Yanga, Paschal Msindo wa timu ya Azam na Haji Abdala kipa wa timu ya Serengeti Boys chini ya miaka 17 iliyoshika nafasi ya pili kwenye michuano ya Afcon ya vijana iliyofanyika Morocco hivi karibuni.

Mbali ya kuzalisha wachezaji hao ambao wanatambulika pia imezalisha wachezaji wengine ambao wako timu za Yanga B, Azam na Fountain Gate pamoja na msanii wa muziki wa kisasa Dogo Janja na wasanii mbalimbali hapa nchini.

Kiluwasha amesema kuwa mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka yanashirikisha jumla ya mikoa mitatu ya Pwani, Dar es Salaam na Morogoro ambapo kuna wachezaji zaidi ya 430 kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Kipaji Changu Mtaji Wangu”.

“Michezo inayoshindaniwa ni pamoja na soka, mpira wa pete, riadha na michezo ya ndani ikiwa ni pamoja na kupiga vyombo vya muziki, ubunifu wa mavi na sanaa mbalimbali lengo ni kuinua na kuibua vipaji kwa vijana,”alisema Kiluwasha.

Alisema kuwa kwa sasa mara wanapopatikana vijana wa michezo husika huwapeleka ili wakaendeleze vipaji vyao ambapo wa soka huwapeleka kwenye timu zenye Academy ili waweze kukuza vipaji vyao na kujipatia ajira kupitia michezo.

“Changamoto kubwa ni ushiriki mdogo wa wadau kujitokeza kuhudhuria mashindano yao pia baadhi ya wachezaji kwenda kushiriki michezo ya Umisseta na Umitashumta kwani nao hufanya kipindi cha likizo hivyo kuwa na mwingiliano,”alisema Kiluwasha.

Aidha alisem akuwa malengo yao ya baadaye ni kuanzisha timu ya mipra wa miguu ili ishiriki ligi mbalimbali na hatimaye kufika ligi kuu pia wanazikaribisha timu mbalimbali kama zinahitaji wachezaji kuona nao ili kukubalina na kuwachukua ili wakaendeleze vipaji vyao.

Wachezaji hao wanatoka kwenye vituo vya huduma ya mtoto na kijana kwenye makanisa ya Kiinjili na Kipentekoste kwenye mikoa hiyo na wachezaji watakaofanya vizuri watachaguliwa kwenda kushiriki mashindano hayo kitaifa.

No comments:

Post a Comment