Ameyasema hayo Mjini Kibaha kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere wakati akifungua Jukwaa la Vijana Uchumi Challenge.
Mapana amesema kuwa Waziri wa Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Joel Nanauka alizindua shindano la vijana kwa ajili ya kuwawezesha vijana nchini Tanzania kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na ubunifu.
"Lengo kuu la mpango huu ni kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia mawazo ya vijana kukuza ubunifu na Ujasiriamali na kuwapa vijana fursa ya kuonyesha mawazo yao ya kibiashara na miradi ya kibunifu inayoweza kutatua changamoto za kijamii na kiuchumi,"amesema Mapana.
Amesema kuwa pia ni kuongeza ajira kwa kusaidia miradi ya vijana kuanzishwa au kukua ambapo shindano linakusudia kupunguza changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kuwezesha vijana kujiajiri na kuajiri wengine.
"Kwa wale ambao hawatafanikiwa kushinda mawazo yao yatachukuliwa na kufanyiwa kazi kwa kupewa mafunzo kutokana na mawazo yao ya bunifu zao kupitia sekta mbalimbali zikiwemo za kilimo uvuvi mifugo tehama na ujasiamali,"amesema Mapana.
Aidha amesema vijana wasilalamike bali watoe mawazo na suluhisho nini kifanyike hata ikitokea changamoto kama za kupanda bei ya mafuta ili uchumi wa nchi uwe stahimilivu
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya Vijana Uchumi Challenge Joseph Malecela amesema kuwa jumla ya mawazo zaidi ya 7,000 ya vijana kote nchini yaliwasilishwa na kuchujwa na kubaki 100 ambayo yatashindanishwa kupata mshindi.
Malecela amesema kuwa washiriki hao 100 ambao wameingia kambini kwenye Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere watachujwa na majaji wabobezi wa masuala ya uchumi na fedha na kubaki 30 na baadaye 10.
Amesema kuwa washindi 10 watakwenda kwenye kilele kitakachofanyika Jijini Dar es Salam Julai 6 ambapo mshindi atapata kiasi cha shilingi milioni 50 huku wapili akijinyakulia shilingi milioni 20 na watatu milioni 10 ambapo vijana wanaoshiriki ni wenye umri chini ya miaka 35.
Kilele kinatarajiwa kufanyika Jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

No comments:
Post a Comment