Na John Gagarini, Kibaha
KIKOSI cha zimamoto na uokoaji mkoni pwani kimewata
wananchikuacha kuuza mafuta aina ya Petroli majumbani mwao ili kuepukana na
milipuko ya moto inayotokana na mafuta hayo ambayo ni hatari.
Hayo yalisema mjini Kibaha na kamanda wa kikosi hicho Goodluck
Zelote alipoongea na mwandishi wa habari hizi na kusema kuwa uuzaji huo wa
kiholela ni hatari kwani umesababisha madhara makubwa ya uharibifu wa mali na
watu kupoteza maisha.
Zelote alisema kuwa uuzaji huu si salama kwani kuhifadhi
mafuta ya petrol ndani ni hatari kutokana na mafuta hayo kuwa ni rahisi kuwaka
hivyo kuyauza kwenye nyumba za kuishi ni hatari sana kwa maisha ya watu.
“Utaratibu wa kuuza mafuta unafahamika lakini kwa sasa
kumeibuka watu kuweka mafuta kwenye madumu pamoja na kwenye chupa za maji kisha
kuyauza kwa madereva pikipiki na mafuta haya huhifadhiwa ndani jambo ambalo ni
la hatari sana kwani watu wamepoteza maisha,” alisema Zelote.
Alisema kuwa mafuta hayo yanatakiwa yawekwe kwenye matenki na
kuchimbiwa chini ndiyo utaratibu unaotakiwa lakini baadhi wanakiuka taratibu
hizo kwa kuyahifadhi kwenye madumu ya maji.
“Tayari tumeshatoa elimu kuhusiana na kuepuka vitu ambavyo
vinachangia moto kuwa majumbani ikiwa ni pamoja na kuepukana na utaratibu huo
pamoja na kutohifhadhi pikipiki ndani ya nyumba kwani ni hatari bali wamiliki
wangeangalia namna ya kuzihifadhi pikipiki zao,” alisema Zelote.
Aidha alisema kuwa bado wanendelea na utaratibu wa kutoa
elimu kwenye maeneo mbalimbali ambayo yana mikusanyiko ya watu kama vile
mashuleni, vituo vya mabasi, mikutano na kwenye masoko kwa lengo la kuwapatia
elimu juu ya kujikinga na majanga.
“Vifaa vya kuzimia moto vinapaswa kuwa kwenye sehemu
mbalimbali za huduma pamoja na majumbani ambapo sheria iko wazi na kuna adhabu
kutegemeana na kosa na ukubwa wa huduma na kuna faini ambayo inaanzia 100,000
au kifungo cha miezi sita,” alisema Zelote.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment