Na John Gagarini, Kibaha
JESHI la Polisi mkoani Pwani linawashikilia Raia 35 wa Ethiopia baada ya kukamatwa wakituhumiwa kuishi nchini bila ya kibali huku likimsaka David Myovela mkazi wa Kilangalanga wilayani Kibaha kwa tuhuma za kuwahifadhi raia hao.
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoani humo Boniventura Mushongi alisema kuwa tukio hilo lilitokea Februari 29 mwaka huu majira ya 5:30 usiku huko Kilangalanga tarafa ya Mlandizi wilaya ya Kibaha.
Kamanda Mushongi alisema kuwa watuhumiwa hao walikutwa nyumbani kwa mtuhumiwa huyo baada ya taarifa kutolewa na wasamaria wema juu ya kuwepo kwa wageni hao ambao walikuwa hawana kibali cha kuishi nchini.
“Wahamiaji hao haramu waliingia nchini wakitokea Mombasa nchini Kenya kupitia mkoa wa Tanga kwa njia ya barabara huku wakiwa kwenye gari la mizigo aina ya Fuso na Noah na kufikia kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo wakijiandaa kwa safari ya kwenda Afrika ya Kusini,” alisema Mushongi.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Tatela Erdadu, Tafesa Tesfaye, Ercuias Hailu, Teseahun Abrahom, Gizochew Bergeno, Meies Kasa, Azole Chebow, Samuel Game, Abtama Falak na Barka Lambamu.
Wengine ni Gazu Abame, Tesk Wark, Gejerm Ababey, Aman Ekdapu, Gadon Hayie, Danak Danel, Tamer Yoanes, Eshey Ayaia , Tasam Ayaia, Tamasoen Dam, Yesak Danei, Gezcho Sugebo, Beramu Make na Abinet Elias.
Aidha aliwataja wengine kuwa ni Mulugeta Abayno, Mehumud Kedery, Mubary Naes, Lmebo Demise, Tamesfen Tadse, Tariku Amato, Tedsue Cueba, Akhelu Moses, Tenekuden Bekeil, Aborome Arizoto, Berhom Kedir ambapo watuhumiwa hao watakabidhiwa kwa idara ya Uhamiaji kwa ajili ya hatua za kisheria.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment