Na John Gagarini, Kibaha
SERIKALI imesema kuwa itaangalia upaya uendeshaji wa Shirika
la Elimu Kibaha (KEC) ili lizalishe liweze kujiendesha kwa ufanisi badala ya
kuitegemea serikali ili kuboresha maslahi ya wafanyakazi wake na kutoa huduma
bora kwa wananchi.
Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Waziri Ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene alipotembelea Shirika
hilo kujionea utendaji kazi wake na na kuongea na wafanyakazi kujua changamoto
zinazowakabili na kusema kuwa linapaswa kujiendesha kwa faida na si kuwa tegemezi.
Simbachawene alisema kuwa Shirika hilo la Umma lilianzishwa
kwa lengo la kusaidia wananchi hasa wale wa vijijini kwa wakati ule lakini
linapasw akubadilika kutokana na wakati na kuacha mifumo ya uendeshaji wa
kizamani ambayo haiendani na hali halisi ya wakati uliopo hivyo kushindwa
kunufaisha watumishi na wananchi.
“Haiwezekani Shirika kama hili lenye rasilimali na vyanzo
vingi vya mapato ikiwa ni pamoja na ardhi kubwa linakuwa na watumishi ambao ni
maskini huku wakikosa stahiki zao za kimsingi na kufanya liyumbe ni jambo la
kusikitisha sana hivyo serikali itakaa na kuangalia njia za kuweza klirudisha
kwenye uhalisia wake,” alisema Simbachawene.
Alisema kuwa Shirika linayumba kw asababu hakuna mipango
mikakati ya kujiendesha kisasa kwani maono yake yanaonekana bado ni ya kizamani
kwa kuendelea kudeka kwa serikali licha ya kuwa na fursa nyingi
zianazolizunguka.
“Mbali ya mfumo wa uendeshaji kuwa na matataizo mengi pia
wafanyakazi wamelalamika sana juu ya maslahi yao ikiwa ni pamoja na malipo ya
kazi z aziada, kupandishwa madaraja na maslahi mengine nitakuja na majibu ya
maswali yenu pia tume itaundwa kila sekta ili kubaini matatizo yaliyopo na
kuyafanyia kazi,” alisema Simbachawene.
Kwa upanade wake mwenyekiti wa bodi ya Shirika Patrick
Makungu alisema kuwa watazifanyia kazi changamoto mbalimbali ambazo
zinawakabili wafanyakazi ambazo zinawafanya watumishi washindwe kutoa huduma
bora.
Naye mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha Dk Cyprian Mpemba
alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinawafanya washindwe
kutoa huduma bora ikiwa ni pamoja na kuwa na mahitaji ya fedha kiasi cha
shilingi bilioni 6.5 kwa ajili ya uendesheaji.
Dk Mpemba alisema kuwa mbali ya changamoto hizo wamepata
mafaniko kupitia mfumo wa kieletroniki wa ukusanyaji wa mapato ya Hospitali ya
Rufaa ya mkoa ya Tumbi ambayo iko chini ya Shirika hilo kufanikiwa kukusanya
kiasi cha shilingi milioni 3,000,000 toka 300,000 kwa siku.
Waziri alitembelea Hospitali hiyo, aliangalia mfumo wa
ukusanyaji mapato wa kieletroniki uliobuniwa na shirika hilo, kampuni ya
ufugaji kuku ya Organia, Shirika hilo lilianzishwa miaka zaidi ya 40 iliyopita na
nchi za NORDIC likiwa na lengo la kupambana na adui watatu ambao ni ujinga,
umaskini na maradhi na lina wafanyakazi zaidi ya 900 na lina miliki Hospitali
ya Tumbi, Chuo cha Waganga wasaidizi, Chuo cha Ufundi Stadi VETA, Shule z a
sekondari Kibaha wavulana na Wasichana, Tumbi, shule ya msingi Tumbi na awali
MWISHO
No comments:
Post a Comment