Na John Gagarini, Kibaha
MADIWANI wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha wanatarajiwa
kusimamia utaratibu wa mapato kwenye stendi kuu ya mabasi ya Maili Moja ili
kuhakiki ni magari mangapi ya abiria yanayolipa ushuru kwenye stendi hiyo.
Utaratibu huo ulipitishwa kwenye baraza la madiwani wa
Halmashauri hiyo ukiwa na lengo la kuhakikisha kuwa fedha zinazopatikana kwenye
chanzo hicho kikubwa cha mapato cha Halmashauri hiyo.
Akizungumza kwenye kikao hicho mwenyekiti wa Halmashauri hiyo
Leonard Mloe alisema kuwa madiwani hao watakaa kituoni hapo ili kupata ukweli
wa magari mangapi yanayolipa ushuru yanapopita hapo stendi.
“Tumeamua kufanya hivyo kwani mapato yanayopatikana kwa sasa
hayana usahihi kwani idadi ya magari yanayolipa ushuru ni machache huku magari
yanayopita hapo ni kubwa hivyo kukaa hapo kutatusaidia kujua ukweli wa mapato
halisi ya stendi,” alisema Mlowe.
Mlowe alisema kuwa wanataka wakadirie mapto kwa uhakika na si
kubahatisha kwani kwa sasa hawaridhiki na mapato yanayopatikana kwa sasa hivyo
wameamua madiwani wake hapo ili kupata majibu sahihi.
“Hichi ni moja ya chanzo chetu cha mapato cha uhakika hivyo
lazima tujue tunapata nini na kujua ni magari ya abiria ni mangapi yanayolipa
ushuru wa stendi kwani iatatusadia kuwa na uhakika wa mapato ya chanzo hicho,”
alisema Mloe.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Tumbi Hemed Chanyika
alisema kuwa mapato ya stendi hayafahamiki undani wake kwani inaonekana baadhi
ya watu wanatumia risiti feki za ushuru wa stendi kujinufaisha.
Chanyika alisema kuwa kwa madiwani hao kukaa hapo itasaidia
sana kwani idadi ya magari ya abiria yanayoingia na kutoka kwenye stendi hiyo
ambapo mabasi madogo yanalipia kiasi cha shilingi 500 na makubwa 1,000 kila
yanapoingia na kutoka.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment