Akipokeaa Tshirt hizo yeye na mke wake katika maadhimisho hayo ya miaka 102 ya kuzaliwa kwa Mwl Julius Kambarage Nyerere lililofanyika katika Ukumbi wa Mji wa Mtumba Mkoani Dodoma tarehe 13.4.2024
Sunday, April 14, 2024
MWAKILISHI WA BALOZI WA UGANDA YAPONGEZA UBUNIFU WA TAASISI YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE MKOA WA PWANI
MEJA JENERALI BALOZI ANSELM BAHATI SHIGONGO ATUMA SALAMU ZA MKOA WA PWANI KONGAMANO LA MIAKA 102 YA KUZALIWA KWA MWALIMU NYERERE DODOMA
MWENYEKITI wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mkoa wa Pwani Mh Meja Jenerali Balozi Anselm Bahati Shigongo amesema kuwa Mkoa wa Pwani ni mkoa bora katika uwekezaji wa viwanda.Mh Meja Jenerali Balozi Bahati ameyasema hayo katika maadhimisho ya kitaifa ya miaka 102 ya kuzaliwa kwa Mwl Julius Kambarage Nyerere yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mtumba Mjini Dodoma tarehe 13.4.2024 maadhimisho hayo yalihudhuliwa na Mh Daktari Philip Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Amewaomba wadau wa maendeleo nchini waende Mkoani Pwani kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
KIMITI AIPONGEZA SERIKALI YA AWAMU YA SITA YA MH DKT SAMIA SULUHU HASSAN RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Kimiti ameyasema hayo katika Maadhimisho ya kitaifa ya kumbukumbu ya miaka 102 ya kuzaliwa kwa Mwl Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Ukumbi wa Mtumba tarehe 13.4.2024 mkoani Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Mheshimiwa Dkt Philip Mpango Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi wengi waliojitokeza kushuhudia Maadhimisho ya kumbukumbu hiyo.
Kimiti amesema kuwa jambo hilo litasaidia kutunza Kumbukumbu za Mwasisi huyo wa Taifa kwa kufanya vijana na makundi mengine kwenda kujifunza pia itaongeza pato la Taifa akiamini watu wa mataifa mengi watakuja kujifunza mambo mbalimbali yaliyofanywa na Nyerere.
Saturday, April 13, 2024
JAMII YAASWA ISILE MALI ZA YATIMA
Thursday, April 11, 2024
SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MFUMO MPYA WA KIELETRONIKI WA UNUNUZI WA UMMA NeST
Na Wellu Mtaki, Dodoma
Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa Mfumo mpya wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma unaojulikana kama National e-Procurement System of Tanzania (NeST) kabla ya uwekezaji huu.
Ununuzi wa umma ulikuwa ukifanyika kwa kutumia mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma uliojulikana kama Tanzania National e-Procurement System (TANePS) ambao ulijengwa na kampuni ya kigeni kutoka Ugiriki lakini Serikali ilibaini changamoto nyingi kwenye ununuzi uliokuwa ukifanyika kupitia mfumo wa TANePS ikiwemo taarifa zote za Ununuzi wa umma kuwa chini ya usimamizi wa kampuni ya kigeni nje ya nchi.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa kujenga uwezo wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Amin Mcharo wakati akizungumza na vyombo vya habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Jijini Dodoma, kuhusu mafanikio makubwa waliyopata katika miaka mitatu ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Amesema kuwa changamoto hii na nyinginezo zilipelekea uamuzi wa kuanzisha mfumo mbadala ambao utakuwa bora zaidi, wenye kuleta tija, unaojengwa na wataalam wa ndani na kusimamiwa na Serikali.
Aidha amewaasa wananchi kujisajili katika mfumoNeST na kuomba zabuni mbalimbali zinazotangazwa na Serikali ili kuweza kujipatia kazi na kuhakikisha anayeomba amekidhi vigezo vinavyotakiwa katika kuomba zabuni husika na pindi wanapopata zabuni wazifanye kwa uadilifu na ufanisi ili waendelee kuaminiwa katika miradi mingine kutokana zaidi ya asilimia 70 ya bajeti ya Serikali inatumika kwenye ununuzi wa umma.
Ikumbukwe kuwa PPRA imekuwa ikitekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kuwahudumia wananchi ili kutimiza lengo la Serikali iliyopo madarakani ya kupeleka huduma kwa wananchi na kuchochea matumizi ya utafiti, sayansi na teknolojia na ubunifu kama nyenzo ya maendeleo, kama inavyoonyesha katika Sura ya kwanza,Kipengele cha 8(e) ya Ilani hiyo wakati sura hiyohiyo kipengele cha 8 (f) ikielezea kujikita katika kutengeneza ajira zisizopungua milioni 8 katika sekta rasmi na zisizo rasmi kwa ajili ya vijana.
Tuesday, April 9, 2024
*WMAs ZATAKIWA KUWA NA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA*
Serikali imewataka viongozi wa Jumuiya za Hifadhi Wanyamapori (WMAs) kuzingatia matumizi sahihi ya fedha ili kuwanufaisha wananchi wa vijiji wanachama pia kuzingatia mikataba inayoingiwa na WMAs hizo kwa maslahi ya Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ametoa kauli hiyo leo Aprili 8,2024 Jijini Dodoma wakati wakati wa kikao cha viongozi wa Jumuiya hizo pamoja na baadhi ya maofisa wanyamapori wa wilaya kuhusu changamoto za usimamizi wa maeneo ya WMAs nchini.
Amesema rasilimali fedha ni lazima zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuendeleza miradi ya maendeleo ya vijiji kwa kuwashirikisha wananchi wa vijiji hivyo.
“Ni lazima muweke mkazo katika kuhakikisha kwamba kunakuwa na uwazi na matumizi sahihi ya fedha pamoja na utoaji wa taarifa kwa wanufaika kwenye vijiji husika, msipofanya hivyo uongozi utageuka shubiri mtakapofanyiwa ukaguzi” Mhe. Kairuki alisisitiza.
Amesema kuwa katika kipindi cha Mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetoa mgao wa takribani bilioni 9.6 ambazo Serikali inaamini zimetumika kwa mujibu wa Kanuni za WMAs ambazo zinaelekeza kuwa sehemu ya fedha hizo zitumike kutekeleza miradi ya maendeleo ya vijiji.
Amesema kupitia kanuni hizo za uanzishaji na uendelezaji wa maeneo ya hifadhi kwa sasa kuna jumla ya WMAs 22 zilizodhinishwa na kupata haki ya matumizi ya rasilimali za wanyamapori lakini kuna nyingine 16 ambazo ziko kwenye mchakato wa kuanzishwa.
Aidha, ametumia fursa hiyo kuzishukuru WMAs kwa mchango wao katika kusaidia kukuza uchumi kwa mtu mmoja mmoja na katika jamii pamoja na kusaidia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika jamii na vijiji wanachama.
“Hii imejidhirishisha katika Sekta ya uwindaji wa Kitalii na utalii wa picha ambapo tumeshuhudia umekuwa chachu ya uchumi kwa vijiji wanachama ambao wanaunda jumuiya zetu” Mhe. Kairuki amesema.
Katika hatua nyingine, Waziri Kairuki alisema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wadau wa uhifadhi imeendelea na jitihada mbalimbali za kuhakikisha Jumuiya zinaendelea kuimarika ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo viongozi wa WMAs kwa lengo la kuimarisha utawala na usimamizi wa maeneo hayo na kuwezesha mafunzo kwa Askari wa Wanyamapori wa Vijiji (VGS) ambapo takribani VGS 540 wamepata mafunzo katika Chuo cha Wanyamapori Likuyuseka – Maganga.
Pia amesema Serikali imewezesha upatikanaji wa vitendea kazi ikiwemo magari ya doria kwa baadhi ya Jumuiya kama Mbarangandu na Nalika, Vilevile, Jumuiya zimewezeshwa vifaa vya uwandani kama vile mahema, GPS, kamera, sare za Askari Wanyamapori wa Vijiji (VGS) na vifaa vya ofisini kama kompyuta katika Jumuiya za MBOMIPA, WAGA na UMEMARUWA.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamishna CP Benedict Wakulyamba, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Fortunata Msoffe ,Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA,wawakilishi wa Makamishna Uhifadhi wa TANAPA, NCAA na TFS, Wakuu wa Idara na Taasisi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Maafisa Wanyamapori wa Wilaya, Wadau wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Viongozi wa Jumuiya za Wanyamapori.
Sunday, April 7, 2024
WASICHANA WATAKIWA KUWA MABALOZI KUPINGA VITENDO VYA UKATILI
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya ukatili wa kijinsia mkoa wa Dodoma Grace Ringo wakati wa mafunzo ya utoaji wa elimu katika chuo Mipango chini ya uongozi wa Binti Makini kuhusu kupinga unyanyasaji kwa wanawake.
Amesema yapo mambo ambayo mwanamke wanakutana nayo kama Ulawiti, kupigwa , pamoja na kukosa haki ambazo zinamfanya mwanamke akashidwa kujiamini katika nafasi yake na kupelekea anguko la uchumi katika jamii hata familia hivyo niwaombe Mabinti ambao mmepata elimu leo muhakikishe mnasaidia jamii
Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya ukatili wa kijinsia Mkoa wa Dodoma Irene Sanga amewasihi Mabinti kutumia mitandao kwa ajiri ya kuwaingizia kipato na sio kutumia mitandao kwa kufanya mambo maovu huku akiwasisitiza wawe na nidhamu Katika jamii ya leo
"Wapo Mabinti ambao wanatumia mitandao kwa kuangalia vitu visivyofaha na kupelekea Vijana kualibika kwa kuiga mambo ambayo kwa nafasi na umri bado na kulazimisha kufanya vitu kama rushwa za ngono," amesema Sanga.
Naye Mjumbe wa kamati ya kupinga ukatili chini ya ofisi ya Mkoa wa Dodoma Rhoda Denis amewataka wasichana kuzingatia kujithamini na kujitambua Ili kujikomboa katika maisha ya jamii ya leo.
"Wapo wanawake wanapigwa na waume zao sababu kukosa kujitambua ila kama utajua thamani yako utaweza kufika sehem ambayo utaweza kupata msaada," amesema Rhoda
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Binti Makini Chuo Cha Mipango Dodoma Swaumu Rajabu amewahimiza wanawake kujitokeza kugombania nafasi mbalimbali za uongozi kwani wanawake tunanafasi kubwa sana katika jamii leo hivyo tuwe mstari wa mbele kuwasihi na wengine unaowaona wanaweza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika nchi yetu .
Aidha amesema kuwa chuo Cha mipango kinaenda kufanyika uchaguzi wa viongozi wa serikali ya wanafunzi ikiwemo nafasi mbalimbali kama Rais wa chuo Cha mipango, wabunge pamoja nafasi nyingine hivyo amewaomba Binti Makini wote wenye sifa wajitokeze wakagombee nafasi hizo.
Ikumbukwe kuwa kamati ya Kupinga Ukatili wa kijinsia iliyochini ya wanawake na Samia inaendelea kufanya mafunzo ya utoaji wa elimu kwa wanawake na wanaume ili kuhakikisha elimu hii inawafikia wengi ili kutengeneza Taifa lenye nguvu kazi na lenye Maadili ikiwa na kauli mbiu IPELEKE DODOMA DUNIANI NA DUNIA ILETE DODOMA
















