Wednesday, September 27, 2023
SHULE SALAMA WAJADILI KUMLINDA MTOTO
TIMU YA NYUMBU YAENDELEA NA MICHEZO YA KUJIPIMA NGUVU YATOKA SARE 1-1 NA POLISI TANZANIA
TIMU ya Soka ya Nyumbu ya Mkoani Pwani inayojiandaa na ligi daraja la Pili imetoka sare ya goli 1-1 na timu ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa Chuo Cha Polisi Kurasini Jijini Dar es Salaam.
Nyumbu huo ni mchezo wake wa pili wa kujipima nguvu ambapo jana ilicheza na timu ya Mashujaa ya Mkoani Kigoma ambayo inashiriki ligi Kuu ya NBC Premium League ambapo pia ilitoka sare ya kufungana goli 1-1 kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya michezo hiyo kocha mkuu wa timu hiyo Rajab Gwamku amesema kuwa anafurahishwa na viwango vya wachezaji wake kupitia michezo hiyo ya kujipima nguvu waliocheza.
Gwamku amesema wataendelea kucheza michezo ya kirafiki zaidi ili kuiimarisha timu yake kabla ya kuanza kwa michezo ya ligi daraja la pili kwa kipindi itakapopangwa kuchezwa ligi hiyo.
Amewaomba Wanapwani kuiunga mkono timu yao ili iweze kufanya vyema kwenye ligi daraja la pili na kupanda daraja la kwanza huku malengo yakiwa ni kupanda ligi kuu ili kuuwakilisha vyema mkoa huo.
WAFUGAJI WILAYANI KIBAHA WABUNI MBINU YA ULINZI KULINDA MIFUGO YSO
KUFUATIA vitendo vya wizi wa mifugo kushamiri Chama cha Wafugaji Wilaya ya Kibaha mtaa wa Mwanalugali kimeweka mkakati wa kutumia ulinzi shirikishi ili kudhibiti vitendo hivyo.
WAFUGAJI KUTUMIA WALINZI SHIRIKISHI KULINDA MIFUGO YAO
Tuesday, September 26, 2023
MAOFISA ELIMU WALIMU WA HISABATI MKOANI PWANI WAPIGWA MSASA
WALIMU wanaofundisha somo la Hisabati Mkoani Pwani wametakiwa kutumia ufanisi umahiri na dhana stahiki kupitia mbinu za ufundishaji wa somo hilo ili kuongeza ufaulu.
Hayo yamesemwa Wilayani Kisarawe na Katibu Tawala (RAS) Mkoa wa Pwani Ramadhan Mchatta ambaye aliwakilishwa na Ofisa Elimu Mkoa Sara Mlaki wakati wa Mafunzo kwa viongozi wa elimu kuhusu uboreshaji ufundishaji na ujifunzaji wa umahiri wenye changamoto katika somo la hisabati kwa mkoa huo.
Mchatta amesema kuwa kumekuwa na changamoto kwa baadhi ya wanafunzi kwenye somo la hisabati ambapo utafiti umebaini baadhi ya wanafunzi kufanya vibaya kwenye mitihani ikiwemo ile ya Mock Wilaya na Mkoa.
Naye mtaalamu kiongozi wa Shule Bora Vicent Katabalo ameupongeza Mkoa wa Pwani kwa kutekeleza vizuri afua mbalimbali za mradi wa Shule Bora na kutaka waendeleze jitihada ili kufikia malengo yaliyowekwa ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi.
Kwa upande wake ofisa elimu mkoa wa Pwani Sara Mlaki amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha umahiri wa wa walimu na viongozi wa Elimu katika kutumia mbinu shirikishi za ufundishaji na ujifunzaji wa somo la Hisabati ili kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi wote.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na Taasisi ya Elimu Tanzania kupitia Program ya Shule Bora ambayo inatekelezwa katika mikoa tisa ya Tanzania Bara kwa Ufadhili wa Serikali ya Uingereza na kwa Usimamizi wa Cambridge Education.
Mafunzo hayo yameendeshwa na wawezeshaji kutoka vyuo vya Ualimu vya Tukuyu na Mpwapwa ambapo washiriki wa mafunzo hayo ni viongozi wa Elimu kutoka katika ngazi ya Mkoa wakiwemo Walimu, Walimu wakuu, Maofisa Elimu Kata, Maofisa Elimu Awali na Msingi kutoka katika Halmashauri tisa na shule teule za Wilaya ya Kisarawe.
Thursday, September 21, 2023
MAAFISA,WAKAGUZI, NA ASKARI POLISI KUTOKA MAKAO MAKUU WANOLEWA NAMNA BORA YA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI
Na, Benedict Mlawa wa Jeshi la Polisi
MSEMAJI wa Jeshi la Polisi Nchini,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP) David Misime amefunga mafunzo ya siku mbili kwa Maafisa,Wakaguzi na Askari wa Polisi kutoka Makao Makuu na Mkoa wa Dodoma.
SACP Misime amewaeleza Askari hao kuwa mafunzo hayo ni mfululizo wa mafunzo yanayotolewa kwa Askari katika Vyuo ndani ya nchi, nje ya nchi na kazini kwa lengo la kuwabadilisha kifikra (mindset change) ili kutoa huduma bora kwa jamii.
SACP Misime amefungua mafunzo hayo Septemba 20, 2023 katika ukumbi wa Polisi Jamii Mkoa wa Dodoma Yakifanyika kwa engo la kuwajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi kwa Nidhamu, Haki, Weledi na Uadilifu.
"Mkibadilika kifikra na kuhudumia wananchi kwa Nidhamu,Haki,Weledi na Uadilifu mtakuwa na uwezo wa kusimama mbele ya wananchi kifua mbele na kwa kutumia Falsafa ya Polisi,wananchi waka waamini na kuongeza imani kwa Jeshi la Polisi ili waoneshe ushirikiano katika kubaini na kuzuia uhalifu".Amesema Misime.
Pamoja na hayo, Misime amewapongeza Askari kwa kushiriki vyema katika mafunzo hayo na kazi kubwa wanayofanya huku akiwataka kwenda kuyafanyia kazi yale waliojifunza ili wananchi waweze kuona mabadiliko ya kifikra na kiutendaji kulingana na mageuzi makubwa yanayoendelea ndani ya Jeshi la Polisi.
Awali akizungumza Mkuu wa Kitengo cha Dawati la Jinsia na watoto kutoka Makao Makuu ya Polisi Kamisheni ya Polisi Jamii Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Faidha Suleiman amewasisitiza Askari wa Kike kuzingatia maadili, kutunza familia, kujijengea uwezo wa kujiamini, kuwa wasafi na kuachana na vyanzo vyote vya mawazo kama vile kujiingiza katika mikopo isiyo na msingi ambayo muda mwingi huwapelekea kuwa ni watu wenye mawazo.
Hata hivyo, ACP Faidha Suleiman ambaye ni mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto Makao makuu ya Polisi amewataka askari kuhakikisha wanafuata na kutekeleza miradi ya Polisi Jamii katika majukumu yao ya kila siku kwani miradi hiyo inagusa kila kitengo cha Jeshi la Polisi.
Amesisitiza katika kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto katika familia zao na jamii kwa ujumla ikiwemo wao wenye kutokujifanyia ukatili.
Naye Mkuu wa Dawati la mtandao wa Polisi wananwake (TPF Net) Makao Makuu ya Polisi Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Eva Stesheni amewataka askari kujifunza namna ya kuandika ripoti ya kazi zao ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi pamoja na kuwasidia katika utunzaji wa kumbukumbu za nyaraka kwa kuwa na mpango kazi ulio mzuri ilikufikia malengo sahihi , Kuwasilisha taarifa, mawazo na kuendeleza ujuzi hasa kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto.
Mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoa wa Dodoma mkaguzi wa Polisi Teresina Mdendemi amewataka askari kutoa huduma bora kwa wateja wa ndani na nje kwani kupitia utoaji wa huduma bora huweza kusaidia kurahisha utendaji kazi wa kila siku na kusaidia katika kupambana na vitendo vya kihalifu hususani unyanyasaji wa kijinsia.
"Tutambue na kufahamu aina ya wateja Pamoja na hisia zao pia tuwe na moyo wa kusamehe kwa lengo la kuimarisha mahusiano mazuri kati ya Jeshi la Polisi na Jamii katika kupunguza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto na vitendo vyote vya kihalifu".Amesesisitiza Mdendemi
Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la Jinsia mkoa wa Pwani Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Eliezer Hokororo amezungumzia Faida na athari ya afya ya akili na kusema kuwa ukiponya akili umeponya maisha yako yote maana akili ni mfumo mzima maisha ya mwanadamu.
Hokororo amesema kwamba watu wengi wameathirika na ugonjwa wa Sonona ambao umetokana na kukosekana na ubora wa afya ya akili na kuchangia kuharibu Fikra, Hisia na Matendo ya mtu kutokana na kutokuwa na afya bora ya akili na mara nyingine kushindwa kabisa kutatua changamoto wananzokutana nazo.
Aidha Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Njombe Mkaguzi msaidizi wa Polisi Wilfred Willa aliwataka askari wa kike kutambua na kuzingatia wajibu wao kwa kuihudumia vyema Familia na jamii huku akisema mwanamke anapaswa kuwa kioo na mwenye tabia njema maana ndiye nguzo kwa jamii.
Picha na Benedict Mlawa wa Jeshi la Polisi
Tuesday, September 19, 2023
ASHIKILIWA KWA KUMWAGIA CHAI YA MOTO DADA WA KAZI
JESHI la Polisi Mkoani Pwani linamshikilia mkazi wa Kwa Mathias Wilayani Kibaha Janeth Dominick (26) kwa tuhuma za kumwagia chai ya moto sehemu mbalimbali za mwili dada wa kazi Filomena Erick (17).