Kwenye mchezo huo ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Mwendapole Kibaha hadi dakika 90 zinakamilika timu hizo hazikuweza kufungana.
Timu hizo zilishambuliana na kukosa magoli hivyo kufanya mwamuzi kumaliza pambano na kuweka penati ambapo Kiduli waliibuka Kidedea na kuingia fainali.
Kwa ushindi huo Kiduli inasubiri mshindi kati ya Mlandizi Soccer Academy na Shamahmad Fc mchezo utakaichezwa kwenye uwanja huo huo wa Mwendapole. Fainali itachezwa Novemba 25 kwenye uwanja huo.

No comments:
Post a Comment