Wednesday, November 11, 2026

MBUNGE ACHANGIA 500,000 UJENZI WA MABWENI SEKONDARI YA MWAMBISI

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka ametoa kiasi cha shilingi 500,000 kwa ajili ujenzi wa mabweni ya Shule ya Sekondari ya Mwambisi.

Koka alichangia ujenzi huo wakati wa mahafali ya 11 ya Shule ya Sekondari Mwambisi iliyopo Kata ya Kongowe Wilayani Kibaha.

Amesema kuwa ili wanafunzi waweze kupata masomo katika mazingira mazuri wadau wanapaswa kuchangia maendeleo ya elimu.

"Mchango uwe chachu ya kufanikisha ujenzi wa mabweni hayo ili wanafunzi wawe kwenye mazingira mazuri,"amesema Koka.

Kwa upande wake mkuu wa Shule ya Sekondari Mwambisi Philemon Fredy amesema kuwa wanashukuru mchango huo kwani utasaidia kuanza ujenzi wa mabweni ambayo tunatarajia kuyajenga.

Fredy amesema kuwa wanatarajia kuanza ujenzi hivi karibuni kwani baadhi ya vifaa tayari wanavyo kwa ajili ya kuanza ujenzi wa mabweni manne kwa ajili ya ujenzi.

Baadhi ya vitu vilivyochangwa ni tofali 2,500 saruji mifuko 33 hivyo kufanya michango yote kuwa na gharama ya shilingi milioni tatu huku bodi ya shule ikiahidi kutoa tofali 3,000.

No comments:

Post a Comment