Thursday, November 5, 2026

MALI ZA SEKTA YA FEDHA ZAFIKIA TRILIONI 10.9

SEKTA ya fedha nchini inaendelea kukua ambapo hadi kufikia Desemba mwaka 2025 jumla ya mali za mfumo wa fedha zimefikia takribani trilioni 10.9.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Mkaguzi Mwandamizi wa Benki kutoka BoT Joel Charles wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya utendaji kazi wa Benki Kuu.

Charles amesema kuwa Benki Kuu ndiyo msimamizi wa taasisi za fedha na imekuwa ikihakikisha wateja wanalindwa.

"Sekta ya kibenki imewekeza asilimia 70 mifuko ya hifadhi ya jamii ni asilimia 23.6 mifuko ya uwekezaji wa pamoja asilimia nne na sekta ya bima ni asilimia 2.4,"amesema Charles.

No comments:

Post a Comment