BENKI Kuu ya Tanzania (BOT) imewataka waandishi wa habari kutoa taarifa za fedha na uchumi kwa usahihi ili wananchi wapate uelewa juu ya masuala ya kifedha kwani ni sehemu ya maisha yao ya kila siku.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) anayesimamia Utawala na Udhibiti wa Ndani Dk Rahma Mahfoudh wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya uelewa wa kazi na majukumu ya BoT.
Mahfoudh amesema kuwa wananchi wanapenda kuelewa juu ya masuala ya kiuchumi pamoja fedha kwani nao ni sehemu ya uchumi.
"Tumieni mafunzo haya ili muweze kuandika habari kwa weledi na kufanya uchambuzi ambao utamwezesha mwananchi kujua masuala ya kifedha,"amesema Mahfoudh.
Naye Meneja wa Idara ya Mawasiliano wa BoT Vick Msina amesema kuwa wamekuwa wakishirikiana na waandishi wa habari kwa kipindi cha miaka zaidi ya 10.
Msina amesema kuwa ushirikiano huo ni pamoja na kuwapatia waandishi mafunzo kupitia Kanda mbalimbali ili kuwajengea uwezo waandishi watoe habari sahihi.

No comments:
Post a Comment