Wednesday, November 11, 2026

WANANCHI PWANI KUNUFAIKA NA HUDUMA ZA AFYA ZA KIBINGWA NA BOBEZI

MKUU wa Mkoa wa Pwani Stanslaus Nyongo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kunufaika na kambi ya huduma za afya za kibingwa na bobezi itakayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani – Tumbi, kuanzia Novemba 16 hadi 20, 2026.

Akizungumza na waandishi wa habari Novemba 11, 2026, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Stanslaus Nyongo, amesema kambi hiyo itatoa huduma za uchunguzi, ushauri, matibabu na upasuaji katika maeneo mbalimbali, ikiwemo magonjwa ya moyo, macho, figo, kisukari, saratani, mifupa, afya ya akili, watoto na magonjwa mengine.

Amesema baadhi ya huduma zitatolewa bila malipo, ikiwemo upimaji wa sukari, uchunguzi wa homa ya ini na upasuaji wa mtoto wa jicho. Aidha, bima zote za afya zitakubaliwa, huku huduma nyingine zikitolewa kwa gharama nafuu zilizowekwa na Serikali.

Nyongo amewahimiza wananchi kujitokeza katika hospitali hiyo kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni. Kambi hiyo itahusisha madaktari bingwa na wabobezi kutoka mikoa ya Iringa, Singida, Morogoro, Pwani na Dodoma, pamoja na Hospitali ya Taifa Muhimbili.
               
mwisho.

No comments:

Post a Comment