Wednesday, November 11, 2026

MBUNGE KIBAHA MJINI KOKA ATOA MILIONI 10 UJENZI OFISI ZA MISIKITI MIWILI

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini Silvestry Koka ametoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa ajili ya ofisi za Misikiti ya Kongowe na Ofisi ya Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Pwani iliyopo Mwanalugali.

Koka ametoa fedha hizo wakati akitoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mariam Abdala mke wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kibaha Mjini Yahaya Mtonda.

Amesema kuwa mahubiri ya Sheikh wa Mkoa Abbas Mtupa ya kutaka watu watoe sadaka kwa ajili ya kumrehemu mtu aliyekufa.

"Mahubiri yaliyotolewa na Sheikh ni muhimu sana tukayazingatia ili tujitengenezee hazina yetu ya baadaye kwani kujitoa kwa ajili ya imani ni jambo jema hivyo fedha hizo zitakwenda kila ofisi moja itapata milioni tano kumtolea sadaka marehemu,"amesema Koka.

Koka amesema kuwa anaungana na familia na waombolezaji kwa niaba ya ofisisi mbunge na kwaniaba ya wananchi wote anatoa pole kwa familia ya Mtonda na pole kwa Chama kwani yeye ni kiongozi na jambo kubwa ni kumuombea marehemu apumzike kwa amani 

Awali akitoa mawaidha Sheikh wa Mkoa wa Pwani Abbas Mtupa alisema kuwa Mungu Mungu kamkirimu Mtonda jambo zito kwani ni mtihani mkubwa na anapaswa kuukubali kwani Mungu kalipanga ila anapaswa kumshukuru.

Mtupa amesema kuwa baadhi ya waumini wanapopata mtihani au tatizo kama hilo hutaka kuishi kwenye ukapera lakini akiamini kuwa limepangwa na Mungu anapaswa kurudi kwenye maelekezo ya mungu. 

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha Dk Nicas Mawazo alisema kuwa jambo hilo ni zito na halizoeleki hivyo waendelee kushirikiana na familia na utaratibu wa rambirambi za madiwani na watumishi wa Halmashauri utaandaliwa baadaye.

Akitoa salamu za familia na Wilaya ya Kibaha Sheikh Said Mtonda amesema wanashukuru kwa niaba ya familia kwa yote yaliyotokea kwa ni mpango wa Mungu 

No comments:

Post a Comment